Kikosi bora cha msimu "VPL" 2015-2016:

Jospina

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,421
1,387
KIKOSI BORA CHA MSIMU "VPL" 2015-2016:

1. Vicent Angban - SIMBA SC
2. Shomari Kapombe - AZAM FC
3. Mohammed Hussein Tshabalala - SIMBA SC
4. Andrew Vicent - MTIBWA SUGAR
5. Paschal Sergie Wawa - AZAM FC
6. Justice Majavbi - SIMBA SC
7. Shizya Kichuya - MTIBWA SUGAR
8. Thaban Kamusoko - YANGA SC
9. Amisi Tambwe - YANGA SC
10. Hamis Kiiza - SIMBA SC
11.Donald Ngoma - YANGA SC

KOCHA - Van Del Pluijm

Kwa mtazamo wangu wapenda soka wenzangu naamini hiki kinafaa kuwa kikosi bora cha msimu huu wa 2015-2016,nikianzia golini kwa ini nimechagua "Vicent Angban" ni mmoja kati ya magoikipa wazuri kwa siku za hivi karibuni na takwimu zinamlinda ndiye kipa aliyefungwa magoli machache zaidi huku akiwa msaada mkubwa kwa timu yake kufika mahala ilipofika.

Upande wa kulia beki namba mbili nimemuweka "Shomari Kapombe" naamini hakuna asiyejua faida ya kuwa na beki dizaini ya shomari,anacheza mpira wa kisasa na hasa amekua mzuri kwenye mifumo tofauti ana uwezo wa kupanda kusaidia na kutengeneza mashambulizi na pia ana uwezo wa kukaba,pia amechangia magoli 7 kwenye magoli ya AZAM FC mpaka kufikia sasa.

Ubavu wa kushoto nimemdondosha "Tshabalala" wa SIMBA SC sababau zipo nyingi ila kubw tu ndiye namba 3 bora kwa msimu huu akiwa amechangia upatakinaji wa magoli mengi ya SIMBA kati ya magoli 43 amehusika kwenye magoli 13 kwa beki anaecheza soka hapa nchini ni kiwango kizuri... najua wengi watahoji kuhusu "Haji Mngwali" jamaa ni mzuri ila majeruhi this time yamemkost sana.

Namba 4 kuna mtu mmoja anaitwa "Andrew Vicent" huyu jamaa anajulikana kwa jina la "Dante" ila maarufu sana "Rasta wa Mtibwa" amekua mchango mkubwa kwa timu ya MTIBWA kufikia mahala ilipofika,amekua kwenye kiwango bora kwa muda mrefu ni tofauti na wachezaji wengine wanaotumika katika namba hiyo.

Namba 5 kamanda mkuu wa idara ya ulinzi ndani ya kikosi cha AZAM FC huyu si mwengine ni "Sergi Paschal Wawa" hakuna ubishi ndiye nguzo muhimu na kuu kwa misimu miwili mfululizo sasa katika kikosi cha AZAM na amekua na kiwango kizuri kwa misimu yote mfululizo.

Kiungo mkabaji nimeamua kumuweka "Justice Majavbi" shujaa asiyeimbwa sana lakini shughuli yake ni pevu sana,amekua msaada mkubwa sana kwa kikosi cha MSIMBAZI ni mchezaji ambaye amekosa michezo miwili tu tangu aingie kikosini,hiyo utaona ni jinsi gani amekua muhimu kikosini.

Winga tereza upande wa kulia wacha nimuweke dogo janja "Shiza Kichuya" anatokea MTIBWA SUGAR nae amekua kwenye kiwango kizuri kwa muda mrefu sana amesaidia na amehusika kwenye mabao mengi sana ya MTIBWA na mwezi uliopita ndiye aliibuka mchezaji bora na isitoshe juhudi zake zimemfikisha hadi timu ya taifa kwa mara ya kwanza.

Kiungo mchezeshaji hapa hakuna ubishi ukibisha basi wewe ni jipu aiseee.. kuna mtu mmoja tu raia wa kigeni ambaye anasumbua sana eneo la kati kwa sasa si mwengine bali ni "Thaban Kamusoko" au al maarufu "Rasta" huyu amekua muhimili mzuri kwenye kutengeneza mashambulizi ya YANGA,pia amechangia upatikanaji wa mabao ya YANGA na kama aitoshi amefunga pia ni mchezaji ambaye amecheza karibia game zote za ndani na nje.

Huwezi kuwa na kikosi bora bila ya kuwa na mfungaji bora,mmoja ya wafungaji bora hapa TANZANIA alishafanya hivyo msimu wa mwaka juzi,ndiye anaongoza kwa kufunga HATRICK niyingi,huyu anaitwa "Amisi Tambwe" mpaka sasa ana goli 20 akivunja rekodi ya msimu uliopita ya mfungaji bora MSUVA,na bado kuna game moja imebaki hivyo tunaweza tarajia chochote toka kwake ila rekodi kubwa bado inashikiliwa na ABDALAH JUMA aliyefunga magoli 25 akifatiwa na BONIFACE AMBANI mwenye mabao 24.

Eneo la Namab 10 nimeamua kuweka wafungaji pacha na ni kama ilivyo kwa tambwe huwezi chagua kikosi bora kisha ukamuacha mfungaji bora,huyu jamaa katengeneza heshima kubwa sana pale MSIMBAZI ndiye kinara wa mabao kwa SIMBA na ndiye mwnye mchango mkubwa sana mpaka SIMBA kufikia pale ilipofika,mpaka sasa ana mabao 19 ukijumlisha na ya ligi ya FA mabao yake 4 anafikisha 23 sio mbaya kwa ligi ya nyumbani kuwa na fowadi mwenye uwezo wa kuvuka idadi ya mabao 20... anastahili kuwepo kikosini.

Huyu jamaa anaitwa "Donald Ngoma" ndiye anahitimisha zoezi langu kwa upande wa wachezaji,amekua msaada mkubwa sana kwa kikosi cha YANGA kwa mechi za nyumbani na nje ya nchi pia,na kizuri kutoka kwake unaweza kumchezesha kama winga anakupa matokea mazuri,ukimpeleka kati ndo usiseme,ukitaka awe msaidizi wa mshambuliaji wa kati napo ni balaa,so kwenye kikosi kama hiki huwezi kumuacha nje mchezaji aina hii,amekua na wastani mzuri wa kufunga na kutengeneza mabao na mpaka sana ana mabao 16.

Namalizia kwa kumchagua kocha atakesimamia kikosi hiki na bila shaka kocha bora huongoza kikosi bora,hapa nafasi naipeleka kwa mzee,kibabu VAN DEL PLUIJM,ni kocha mzoefu kwa ukanda wa AFRIKA amekua msaada mkubwa kwa YANGA tangu alipokuja mara ya kwanza kisha akaondoka na sasa amerejea tena lakini makali ni yale yale,ni kocha ambaye anapenda muda wote timu ishambulie tu hata kama mpo ugenini mnacheza na timu bora.
 
I

hapo kwa angban waka manula,huko mbele umeweka goalsgetter watupu timu haitakuwa na balance
 
List nzuri, lakini mtazamo wangu pale kwa golikipa, ningemweka Aishi Manula, amekuwa na kiwango kizuri sana mwaka huu toka ligi inaanza kuliko Angban ambaye alianza kufanya vizuri baadae kabisa.

Aidha yule Andrew Vincent naye alijitahidi lakini sidhani kama anaweza kumweka benchi Kelvin Yondamn
 
Yanga ambayo defence yake imeruhusu magoli kidogo kuliko timu zote haina hata mlinzi mmoja. Hii si kweli
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom