Kikao cha familia

Hussein J Mahenga

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2012
Posts
756
Reaction score
660
KIKAO CHA FAMILIA.
Na.
Uncle Kaso
___________
"Nimewaiteni wanangu, kwa mapenzi mujarabu niliyonayo kwenu". Baba alisema kwa sauti ya upole kabisa.

Wakati huo, mimi na Damary tulikuwa tumekaa kimya nyuma kidogo ya mkusanyiko huo wa familia. Nakumbuka vizuri kabisa ilikuwa ni majira ya saa tatu na nusu usiku, tukiwa tumekaa kuzunguka moto kama ilivyo ada ya jamii za kisukuma. Hatukutaka kuongea chochote kwani aliyokuwa ameyafanya baba, hakika hakuna aliyekuwa kapendwa nayo ila kaka yetu Kitunda. Kiukweli tulimchukia sana na kila mmoja wetu alijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu, kwa nini kaka yetu alionekana kuwa karibu sana na baba hali ya kuwa matendo ya baba yalimkera si mama tu, bali karibu kila aliyekuwa akiishi hapa nyumbani.

Wakati akiendelea kuzungumza, Damary, mdogo wangu aliniambia kwa sauti ya chini, " baba asipotengua kauli yake, nitaenda mbali na wala sintorudi tena". Maneno haya yaliuchoma moyo wangu, lakini kwa kuwa aliyekuwa ametukosea ni baba yetu, hatukuwa na budi kuvumilia kwani wahenga walisema, mkubwa hakosei.

Matarajio ya kikao kile yalikuwa makubwa kwa upande mmoja, japo mimi na Damary tulikuwa tumeshakata tamaa kabisa kabisa. Tulikaa pale kana kwamba ni mdori uliowekwa dukani kuvutia wateja.

Wakati akiendelea kuzungumza akiwa amekaa kwenye kiti chake, mara kwa mbali nilimuona Masudi ambaye yapata siku kumi zilizopita waligombania tape ya makhirikhiri ambayo hakika ilikuwa imepangwa kuchezwa siku ha harusi kaka yetu Malale.

Baba yetu ni mkuu wa sungusungu. Vilevile ni mwenyekiti wa kijiji cha Nsanga. Kijiji hiki kina watu aina mbalimbali. Wapo wakulima, wafinyanzi, wasusi, wawindaji, viongozi wa mila na waendesha unyago. Baba yetu mara nyingi alisema ni lazima tuishi katika umoja ili kukifanya kijiji chetu kuwa cha mfano wa kuigwa na vijiji vingine. Katika jamii za kisukuma, tulikuwa na mgawanyo wa maeneo ya kiutawala ambapo tulikuwa na magunguli. Ndani ya magunguli, wananchi walifanya shughuli mbalimbali za kijamii kama kushirikiana katika mazishi, harusi na wakati mwingine hata katika shuguli za kilimo. Kwa hiyo, katika kijiji cha Nsanga, kulikuwa na magunguli tisa, na moja ya gunguli lilikuwa ni Itanana ambapo baba alikuwa amemteua kaka yetu mkubwa kuwa mkuu wa gunguli.

Kwa kuwa maamuzi ya baba yaliheshimika na wengi, wachache ambao walionekana kuyachukia maamuzi haya ya kumchagua kaka kuwa mkubwa wa gunguli, aidha aliitiwa sungusungu ama alicharazwa bakora waziwazi na sungusungu ambao walikuwa ni walinzi binafsi wa baba. Kwa hiyo, pamoja na kuwa utaratibu haukuwa hivyo, baba aliamua kumpa sungusungu wawili wa kumlinda kaka kwa usalama wake.

Kaka alitumia upendo wa baba kunyanyasa watu. Alitoa amri binafsi mbalimbali hata kama ziko nje ya utaratibu wa gunguli hilo. Wanakijiji walishangaa sana kuona kwa nini baba yetu alionekana kumpenda kaka hata kama alionekana kukosea.

Nakumbuka siku moja tuliarikwa kwenye sherehe ya unyago. Baba alisimama mlangoni mwenyewe akikagua alama mkononi zilizowekwa kwa wino kama kitambulisho. Kaka siku hiyo hakuwa na alama hiyo, lakini aliingia kwenye sherehe ile. Wanakijiji walipiga kelele lakini wapi. Tulipoanza kula, kila ambaye mikono yake ilikuwa michafu, baba alimtoa na kumsisitiza akanawe tena mikono itakate. Wengine walipotoka, walitoka jumla, kwani mikono yao ilikuwa imeshika gundu ambayo ilikuwa ni ngumu kuitoa kwa maji. Kaka yangu pia alikuwa ameshika gundi, lakini alikula!

"Baba, hata huyu ni mchafu!". Damary alipiga kelele akijaribu kumzuia kaka asimege tonge wala kuchukua nyama. Wanakijiji pia, waliokuwa wametolewa wakiambiwa wachafu, walipaza sauti zao kumlalamikia kaka yangu ili naye akanawe, lakini cha ajabu, baba hakumwambia chochote. Badala yake alisema kwa saui kubwa kabisa, " Malale, we kuka ushibe uwahi nyumbani". Watu wote walitoa macho kana kwamba ni panya aliyebanwa na mlango.

Sasa, siku wanagombania ile tepu na Masudi, kaka yangu alikuwa amepanga ichezwe siku ya harusi. Masudi yeye alikuwa na redio kaseti ambayo wengi waliiazima ili kusherehesha sherehe zao.

Masudi hakutaka kuicheza tepu ile kwani nyimbo zilizokuwemo zilikuwa za matusi na hazikuwa na maadili. Alipokataa, kaka akiwa na sungusungu wawili, alienda kwa Masudi usiku. Sungusungu wale walikuwa na marungu na mijeledi. Kaka alitoa amri moja tu kuwa, anaitaka tepu ile ichezwe. Ilikuwa ni fujo kwa Masudi.

Kesho yake, Masudi alienda kumshtaki kwenye kibanda cha sungusungu mkuu. Usukumani, huwa tuna kitu kinachoitwa *ndege ya hase*. Hiki ni kikundi kinachopewa jukumu la kupeleleza tukio. Kikosi hiki kiliagizwa kwenda kupeleleza tuhuma za Masudi na kikajiridhisha kuwa, ni kweli kaka alienda pale usiku.

Kwa kawaida, kikundi hiki huwa hakitoi taarifa mpaka kimhoji na mlalamikiwa. Kilienda mpaka kwa kaka, lakini kaka alipokiona kikosi hiki, alitokea mlango wa nyuma ya kibanda chake.

Wakati anaendelea kuongea, kumbe Masudi naye alikuwa anakuja kwenye kikao kile. Hatukujua ujio wake ulikuwa ni wa taarifa, au kwa mapenzi yake na baba yangu? Lakini, anawezaje kuwa na mapenzi na baba yangu wakati wana ugomvi na kaka yangu?

Alipogeuka nyuma, baba alimuona Masudi akiwa karibu kabisa na kaka.
"Masudi, njoo hapa." Baba alisema. "Na wewe Malale njoo hapa"..

Kila mtu alibaki kushangaa na wengine wakawa wananong'ona kwa chinichini.
" We Malale, mrudishie Masudi tepu yake na msigombane tena!".

Kiukweli hakuna aliyeamini busara za baba yangu. Karibu familia nzima na majirani walishangilia. Kikao cha familia kiukweli kilikuwa na manufaa makubwa. Mimi na Damary tulibaki kuangalia. Na baadae, baba alifunga kikao akiwaacha Masudi na Malale wakiwa wameshikana mikono, huku Masudi akionekana kuangakia pembeni kana kwamba hakuwa tayari kukubali busara za baba yangu.

Uncle Kaso
 
Hahahaha huyu baba anambichwa mbaya sana.Ujue mpaka sasa wanafamilia waliokuwa wanamkubali tumeanza kumchukia ukiacha upendeleo kwa kaka lakini pia baba ananiudhi na tabia yake ya visasi na kukomoa wasiomkubali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama damary hajaolewa naomba namba yake mkuu,naweza mpa hifadhi ya muda.

Ila malale ana shepu la haja.
 
Nimeshindwa kusoma mkuu, badili rangi. hii inazingua kusomaaa
 
Asante kwa kuweka wazi tatizo la baba kumlea kaka hata pale anapoonekana amekosea, hali hiyo imesababisha wanakijiji kuhisi baba anauhusiano usio wa kawaida na kaka wengine wamefikia kusema kuna imani za kishirikina zimehusishwa eti baba anamla tigo kaka kisiri ili mambo yaende sawa.

Hii tabia ya kutopenda kushauriwa na watoto wake hata wanakijiji ni mbaya kwani sasa kila mtu anaogopa kumuambiwa ukweli hata pale anapokesea kwa sababu ya ile kauli yake ya Msinipangie cha kufanya aliyoiongea kwa kufoka tena hadharani kwenye kikao cha kijiji.
 
nimecheka sana.
 
Najua kuna mtu atakuja hapa atakuambia weka audio..eti wavivu kusoma..
 
Na huyu mkuu wa Gunguli Akiendelea kutopokea ushauri IPO siku KAKA atamponza,HAWA sungusungu wanaomlinda Kaka na BABA hawataweza kuzuia fujo za wanakijiji
 
Hiyo tape ndo flash ya makonda aliyokomalia Ruge? makonda/kaka ndo kapewa ulinzi binafsi wa sungusungu na kupendelewa na baba?
Ujue umezingua sana Uncle Kaso!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…