Kikao cha Bunge chaanza leo

Ufunuo wa Yohana

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
318
67
MASWALI 210 KUJIBIWA
MISWADA 16 KUWASILISHWA
ZITTO STOP TENA STOP

2007-10-30 10:22:35
Na Richard Makore, Dodoma


Kikao Cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa?Tanzania kinaanza leo mjini hapa ambapo miswada 16 ya sheria inatarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa na wabunge.

Akizungumza na wandishi wa habari?mjini hapa jana Ofisa Habari Mkuu wa?Bunge,?Bw. Ernesti Zulu alisema, kikao hicho kinachoanza leo kitamalizika Novemba 16 mwaka huu.

Alisema jumla ya maswali 210 yataulizwa na wabunge na kujibiwa na upande wa serikali.

Aidha, Bw. Zulu alikanusha madai kuwa Mbunge machachari wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA)?Bw. Ztto Kabwe amesamehewa adhabu na hivyo ataweza kuhudhuria kikao cha leo.

Alisema wabunge wakishatoa adhabu kwa mwenzao hakuna haja tena ya mhuisika?kupewa barua ya kusimamishwa kuhudhuria kikao cha bunge.

Awali kulikuwa na? madai kwamba Bw. Zitto angeweza kuhudhuria kikao hicho kwa kuwa alisimamishwa kazi kwa? madai ya kusema uongo bungeni bila barua.

Kutokana na kutopewa barua rasmi kulitolewa madai ya kwamba Bw. Zitto angeweza kuonekana tena Bungeni na hivyo kufutwa kwa adhabu aliyopewa.

``Mbunge akipigiwa kura za kusimamishwa kuhudhuria kikao cha Bunge na wabunge wenzake hakuna haja ya kupatiwa tena barua hivyo Bw. Zitto bado anatumikia adhabu yake,`` alisema Bw. Zulu.

Bw. Zulu alisema maandalizi yote ya kikao hicho yamekamilika na Wabunge tayari wapo mjini hapa.
 
Back
Top Bottom