singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
Na. Ahmad Mmow, Kilwa-LINDI.
Uhifadhi wa msitu katika kijiji cha Nanjirinji A, wilayani Kilwa mkoani Lindi, umeendelea kuwanufaisha wananchi wakazi wa kijiji hicho baada ya kuanza kuwapatia ruzuku akina mama wajawazito wanaoishi katika kijiji hicho.
Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Jafari Nyambate, mwanzoni mwa wiki iliyopita alipozungumza na Lindiyetu.com mjini Kilwa masoko.
Nyambate alisema baada ya kutekeleza miradi mbalimbali ya jamii kwa kutumia fedha zilizotokana na mauzo ya mazao ya msitu waliohifadhi, unaofahamika kwa jina la Mbumbila, Kijiji kimeanza kuwapa ruzuku ya shilingi 30,000 akina mama wajawazito wakazi wa kijiji hicho.
Ikiwa ni mchango wa maandalizi ya gharama za matibabu wakati wakujifungua.
“Fedha hizo zinatolewa kwa mama ambaye mimba yake imefikisha umri wa miezi tisa, muda ambao anatarajia kujifungua ili aweze kufanya maandalizi ikiwamo kununua vifaa vitakavyotumika wakati huo,”alisema Nyambate.
Alibainisha kuwa huo nimwendelezo wa huduma mbalimbali za jamii zilizotekelezwa kutokana na mapato ya msitu huo. Ambapo baada ya kufanikiwa mpango huo,wanajipanga kuanza kutoa ruzuku kwa wazee wasiojiweza.
Mwenyekiti huyo aliitaja baadhi ya miradi iliyotekelezwa kutokana na mapato ya msitu huo kuwa ni vyumba vi 3 vya madarasa ya shule ya msingi, visima vifupi 7 vya maji, soko, vyoo vya kudumu vya shule ya msingi vyenye matundu 6.
Aliitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na nyumba moja ya mwalimu, madawati 26, bomba la maji la shule na viti 100 vinavyotumika wakati wa mikutano mikuu ya kijiji.
Hata hivyo pamoja na mafanikio hayo, mwenyekiti huyo alisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali. Ikiwamo uvamizi unaofanywa na wakulima, hasa wa zao la ufuta ambao wanalazimisha kuendesha shughuli za kilimo ndani ya msitu waliouhifadhi.
“Lakini pia wapo wanaopasua mbao kwa njia haramu, nao wanatusumbua sana ila tunakabiliana nao kwa kufanya doria za mara kwa mara, hasa baada ya kamati ya maliasili kuwezeshwa pikipiki tatu zinazotumika kwa doria,” aliongeza kusema.
Uvunaji katika msitu huo wenye hekta 61724, ulianza rasmi mwaka 2012