Kijana kuamini huwezi toboa bila uchawi, umaskini wako unaanzia hapo

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
Ni mambo ya Ajabu kijana tunayeamini umeelimika bado mpaka leo unawaza pesa za majini.
Unawaza bila kwenda kwa mganga Bishara yako haitakaa,
Unaamini bila kutoa kafara hutapata pesa..
Unawaza bila kuwekewa zindiko hutodumu...

Ukiumuuliza ana ushahidi flani, atakuambia oo sijui tajiri flani ana majoka nyumbani kwake, mara anakambuzi kake kampiga show, mara Analala chini, Kila siku lazima azimie, Akilala anakufa kwanza anaoza, Kamuua Mama yake..
Mwingine Anakuambia yote haya ila hana ushahidi, Utasikia na yeye kaambiwa.

Yaani mambo mengi ya ajabu ajabu, Sasa hata kama ni kweli kwahio wewe unaona hizo njia ni sawa?
Huo utajiri una raha gani kwa mateso na mashrti hayo?

Na ukishaamini katika hilo, kila utakapokwama utaona kuna mkono wa mtu, utapoteza muda mwingi sana kutafuta waganga kumbe nao wanakulia pesa zako..

Jiulize, hivi katika maisha yako huna ushaidi wa ndugu/rafiki au jamaa aliyefanikiwa huku ukimuona aki hustle from the scratch?, kwa nini usiamini kwa wale waliofanikiwa zaidi basi ni hustle zaidi na bahati?
 
SISI WENGINE KUMPATA YESU TU TUSHATOBOA HAYO MENGINE ZIADA (TUMAINI NI YESU)
a0478b9c-f6e2-4877-908e-d4822b371455.jpg
 
Nasimama na wewe mkuu.

Japo wengi watachukia ila nitaongezea, pia kumuamini mungu(dini) ni chanzo cha umasikini. Nimebaini hili kutokana na kigezo kwamba kanda maskini kuliko zote duniani(Sub-Saharan Africa) ndo kanda iliyoshika dini kuliko zote duniani.

Pamoja na Latin America, na Middle East.

Middle East yote sio fukara, ila ina machafuko mno yanayotokana na hitikadi za kidini.

Nataka kusema nini? Dini inafifisha mitazamo ya watu. Kila kitu kinachukuliwa katika vigezo viwili; mwanga na giza. Kwa namna hiyo kuna mengi ya msingi yanapuuzwa(au tuseme elimu dunia)
 
Una hoja
 
Ni mambo ya Ajabu kijana tunayeamini umeelimika bado mpaka leo unawaza pesa za majini.
Unawaza bila kwenda kwa mganga Bishara yako haitakaa,
Unaamini bila kutoa kafara hutapata pesa..
Unawaza bila kuwekewa zindiko hutodumu...

Ukiumuuliza ana ushahidi flani, atakuambia oo sijui tajiri flani ana majoka nyumbani kwake, mara anakambuzi kake kampiga show, mara Analala chini, Kila siku lazima azimie, Akilala anakufa kwanza anaoza, Kamuua Mama yake..
Mwingine Anakuambia yote haya ila hana ushahidi, Utasikia na yeye kaambiwa.

Yaani mambo mengi ya ajabu ajabu, Sasa hata kama ni kweli kwahio wewe unaona hizo njia ni sawa?
Huo utajiri una raha gani kwa mateso na mashrti hayo?

Na ukishaamini katika hilo, kila utakapokwama utaona kuna mkono wa mtu, utapoteza muda mwingi sana kutafuta waganga kumbe nao wanakulia pesa zako..

Jiulize, hivi katika maisha yako huna ushaidi wa ndugu/rafiki au jamaa aliyefanikiwa huku ukimuona aki hustle from the scratch?, kwa nini usiamini kwa wale waliofanikiwa zaidi basi ni hustle zaidi na bahati?
Nikipata pesa za moto naenda kuchukua
 
Nasimama na wewe mkuu.

Japo wengi watachukia ila nitaongezea, pia kumuamini mungu(dini) ni chanzo cha umasikini. Nimebaini hili kutokana na kigezo kwamba kanda maskini kuliko zote duniani(Sub-Saharan Africa) ndo kanda iliyoshika dini kuliko zote duniani.

Pamoja na Latin America, na Middle East.

Middle East yote sio fukara, ila ina machafuko mno yanayotokana na hitikadi za kidini.

Nataka kusema nini? Dini inafifisha mitazamo ya watu. Kila kitu kinachukuliwa katika vigezo viwili; mwanga na giza. Kwa namna hiyo kuna mengi ya msingi yanapuuzwa(au tuseme elimu dunia)
Mchawi..!
 
Kwani tatizo liko wapi ? 😅Kila mtu ana imani yake kama wewe umetoboa sana ebu tuonyeshe jina lako katika matajiri wakubwa hapa bongo.

Kuna mwenzio anakucheka nae kafanikiwa kwa njia hizo ,kila mtu ashinde mechi zake ...Kama hauna imani ni vizuri zaidi ila wanaoamini waache ... Finally mafaniki yataamua .

Yale mazishi aliyofanyiwa malkia Elizabeth ule ni uchawi tosha tu kuamini haya mambo yapo ,japo hakuna uhusiano wa moja kwa moja na mafanikio.

Hakuna anayejua yote kuhusu dunia hapa tunaishi na kuishia.
 
Ulishawahi kujiuliza kwanini graduates wengi wanapoanzisha biashara huwa hazimalizi hata miezi nane zinakufa? Tena wengine wamesomea uhasibu, business administration na marketing kabisa, ulishawahi kujiuliza why waastafu wakipata kiinua mgongo wakianzisha biashara wanaishia kufilisika? Ulishawahi kujiuliza kwa nini muha wa kigoma muuza maji akifungua duka halifi? Au kwanini mchaga na usomi wao wote huwa wanaenda kilimanjaro kila mwisho wa mwaka? Ulishawahi kujiuliza wanaendaga kufanya nini ? Na kwanini huwa hawasemi yanayoendelea huko? Ulishawahi kujiuliza kwanini biashara zao hua hazifi kizembe? Ulishawahi kujiuliza kwanini kwenye maduka ya wahindi ukienda utakuta wanachoma ubani au udi asubuhi? Ulishawahi kujiuliza kwanini simba ya mo dewji kijana msomi timu yake iliingia na moto uwanjani huko afrika kusini? Ulishawahi kujiuliza kwanini biashara nyingi zinakufa licha ya kuwa na mtaji na kuwa ktk location sahihi ? Ukiyapata majibu basi jua kuna elimu ya kitaa ambayo haisomewi inaitwa KITAOLOJIA.
 
Hao hao vijana unaowaambia wasiamini uchawi, hawatapa pesa.

Upande wa pili Vijana hao hao Ndio wanapata pesa kwa kujiita wachawi na waganga...

Ni Yeye kijana kuchagua Kua Mtafuta Uganga, au KUJIITA mganga.

Kuna fundi mzuri sana wa finishing alishanifanyia kazi, nakumbuka wakati ananifanyia hio kazi alikua kaajiri madogo kama 10 hivi,

Yupo vizuri sana hasa kwenye uundaji wa huu mpya wa kisasa wa hizi Board za juu mbadala wa Gypsum na singboard, wanatengeneza kwa kutumia mkonge na Powder inakua strong sana, showcase za tv n.k, sijui kitaalam wanaitaje.

Shida moja alikua tapeli sana, amekula sana pesa za ufundi kwenye Magorofa ya watu Dar..

Baada ya kuingia kwenye Msako akakimbilia Amani tanga na Korogwe kwa msisi..

Miezi kadhaa iliyopita nilikua napita maeneo ya Soni Bumbuli, nikamuona Pale stendi, Nikamwambia kuna mtu ana kazi, nilikutafta sana sijakupata..

Akaniambia Nimeacha, Asaivi mimi ni mganga wa Mali, majini n.k mpaka jina na dini nishabadili.

Nilichokaa, yaani nikavuta picha ule utapeli wake wa kwenye ufundi, alishaenda mpk Germany,akarudi kwa utapeli, katapeli Makanisa, yaani anaenda kwa pastor anampanga anapanda Madhabahuni anahubiri halafu anatumia fursa hio kutangaza kama ana kampuni ya Ujenzi waumini wanajaa, mashule n.k leo hii kahamia huku?

Watu kuigia king kwake ni rahisi sanaa,
Kwanza anaweza kuongea, anushawishi, wengine wanajaa kwenye 18 kwa muonekano, ukimuona ni kama Boss flani hivi, wakati namuona nilivyoambiwa ni fundi Sikuamini,

Mimi pona yangu ni kwamba ndio wa kwanza, hivyo Alitumia Kazi yangu kama Sehemu ya Matangazo, Alipiga kazi kila mtu akitaka anamuonesha Hio..

Sasa nikamuuliza huko kwenye uganga imekuaje? Akaniambia tuu "kule hakuna pesa kama huku, huku hakuna kushatkiwa, maana hatuiti utapeli, tunaita imani, huwezi kushakiwa kwa muujiza kutotokea"

Nikamuambia, mi rafiki yako, niambie ukweli, Hio kitu ni kweli ipo? Akacheka akaniambia,
"hapa nimekuja kuchukua pesa ndio narudi, kuna mtu alikuja dili lake limetiki kaniita kunishukuru, SIJUI HATA IMEKUAJE ila kupitia watu kama hawa wachache ndio tunapata pesa na wateja."
Aliongea mengi ila daa, nimegundua kuna watu wanafanikiwa ila haamini kama amefamikiwa sababu yake mwenyewe na baraka nyingine anaamini aliyemfanikisha ni mganga.

Mwisho wa yote, uwoga/kutojiamini na mteremko ni chanzo cha yote.
 
Kwani tatizo liko wapi ? 😅Kila mtu ana imani yake kama wewe umetoboa sana ebu tuonyeshe jina lako katika matajiri wakubwa hapa bongo.

Kuna mwenzio anakucheka nae kafanikiwa kwa njia hizo ,kila mtu ashinde mechi zake ...Kama hauna imani ni vizuri zaidi ila wanaoamini waache ... Finally mafaniki yataamua .

Yale mazishi aliyofanyiwa malkia Elizabeth ule ni uchawi tosha tu kuamini haya mambo yapo ,japo hakuna uhusiano wa moja kwa moja na mafanikio.

Hakuna anayejua yote kuhusu dunia hapa tunaishi na kuishia.
NAKAZIA HAPA
 
Back
Top Bottom