Chances za kila kijana kukutana na mtu mwenye pesa japo haujataja kiwango ili ajipendekeze ni kiasi gani?
Kwa mfano mimi ni afisa mdogo sana, lakini kuna watu huwa nawapa tenda za hapa na pale zinazowapatia na wao ulaji basi wananiita Bosi, japo ni jina ambalo sipendi kumuita au kuitwa na mtu yeyote maana naona limekaa kinafki nafki sana.
Maana hata mwajiri wangu siwezi kumuita Bosi.
Swali la kupata uelewa tu. Hivi kuna wanawake wanaojipatia pesa kwa kujishusha na kujipendekeza kwa wanawake wenzao kama wanavyofanya hao uliowatolea mfano?Hilo ni jambo la kawaida. Tatizo sio kuitwa “Bosi” au kumpa mtu heshima tatizo ni pale unapojishusha, unajipendekeza au kusifia mtu kama yule Jamaa dalali mwenye manywele na yule mtangazaji wa radio fulani wale vijana lengo lao nikupata manufaa. Heshima iwe ya kweli, sio biashara ya maslahi na kujidhalilisha
Mkuu rudi na usome paragraph ya kwanza ile mistari nane ndio imebeba dhima ya uzi wote huuSwali la kupata uelewa tu. Hivi kuna wanawake wanaojipatia pesa kwa kujishusha na kujipendekeza kwa wanawake wenzao kama wanavyofanya hao uliowatolea mfano?
Naelewa utakaa sawa usijaliNipo busy kidogo maana sikuwa vizuri kiafya, ile thread yako kule Jamii intelligence nimepata mifano mingi sijapata muda wa kuiandika ili wadau tuone mawazo yao
Mkuu, pale umegusia vijana kwa ujumla wao. Lakini trend inaonesha vijana wa kiume ndio flag bearers kwenye hiyo sekta ndio maana nimetamani kufahamu kwa jinsia ya kike hali ipoje.Mkuu rudi na usome paragraph ya kwanza ile mistari nane ndio imebeba dhima ya uzi wote huu
Hahaha nakumbuka enzi zetu kabla ya JK kuchukua nchi watu tulikuwa tunatembea na Mavitabu ya Barnet, Abbott 🤣Taaluma isipokaa vizuri, lazima iathiri uwezo wa vijana katika kufikiri. Leo hii vijana hawachambui vitabu vile vikubwa (tulikuwa tunaita mikate), matokeo yake wanajikita kwenye kukariri maswali, maswali yakijirudia tayari ana division I
Ujumbe huu una hoja nzito sana. Kiini chake ni kwamba heshima, unyenyekevu na kuomba msaada si sawa na kujipendekeza au kujidhalilisha.Vijana wengi leo wanapoteza nguvu zao katika kutafuta kukubalika na watu wenye fedha, madaraka na ushawishi. Badala ya kujenga uwezo wao, wanatumia muda mwingi kujipendekeza, kusifia kila kitu kinachofanywa na mtu mwenye uwezo na hata kuvumilia kudharauliwa kwa sababu tu wanatumaini siku moja watapata msaada.
Huo si mkakati wa maisha.
Kumheshimu mtu mwenye mafanikio ni jambo jema. Kujifunza kutoka kwake ni jambo la busara. Kuomba msaada unapohitaji ni sehemu ya maisha. Lakini kujishusha thamani ili upate nafasi katika maisha ya mtu mwingine ni jambo tofauti kabisa.
Usiwe mtu anayehitaji kila mara kuthibitisha thamani yake mbele ya mwenye pesa. Usibadili misimamo yako kwa sababu tu mtu fulani ana uwezo wa kifedha. Usimsifu mtu kwa kila jambo hata pale unapojua amekosea, kwa sababu tu unaogopa kupoteza faida unayoipata kwake.
Jenga kitu ambacho ni chako.
Jenga mahusiano yenye afya.
Jenga uwezo wa kufikiri.
Jenga jina lako kwa uadilifu.
Maisha yanaweza kuwa magumu, lakini ugumu wa maisha usikulazimishe kuuza heshima yako.
Kuna tofauti kubwa kati ya unyenyekevu na kujipendekeza. Kuna tofauti kati ya heshima na uchawa. Kuna tofauti kati ya kuomba msaada na kuwa tegemezi wa huruma za wengine.
Kijana mwenye kujiamini hawezi kudharau wengine kwa sababu hawana fedha, lakini pia hatajidhalilisha mbele ya mwenye fedha kwa sababu tu ana pesa.
Jifunze kuingia kwenye chumba ukiwa na kitu cha kuongeza mezani, si mikono miwili tu iliyonyoshwa kuomba.
Na kama leo huna kitu, usiione hali hiyo kama hukumu ya maisha yako. Itazame kama hatua ya safari. Jifunze, fanya kazi, anza kidogo, jenga mtandao wa watu sahihi na endelea kusonga mbele.
Usitafute watu wenye pesa ili uwatumie; jenga uwezo ambao siku moja utakufanya wewe uwe mtu ambaye wengine wanakuja kwake kwa thamani unayoleta.
Kumbuka:
Heshima ya kweli haijengwi kwa kujipendekeza. Inajengwa kwa tabia, uwezo, uadilifu na thamani unayoweka katika maisha ya wengine.
Usiwe chombo cha mtu.
Usiwe kivuli cha mtu.
Usiishi kwa kutafuta makofi ya watu.