Hii ilitokea tukiwa jeshini Mlalakuwa (Ujenzi). Afande mmoja alinikuta tukiwa tumejificha nyuma ya kibanda cha choo na wenzangu wawili ambao tulikuwa tumepokelewa wiki hiyo tu tukiwa tumetokea 836 KJ ambako tulitoroka. Yule afande aliyekuwa na cheo cha koplo akang'aka kwa masikitiko. " Nyie watu mmetoka Mgambo bila Movement (akiwa na maana movement order) tumewapokea. Sasa mnakuja kujificha huku, mkipata matatizo nani atakuwa possible, si mimi bana?" mwisho wa kunukuu.