Kigwangallah alishawahi kumkaimu Rais

Kigwangallah alishawahi kumkaimu Rais

maatope

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2013
Posts
1,422
Reaction score
957
Yes, huyu jamaa alishawahi kuitawala Tanzania kwa dakika kadhaa baada ya Mr Kikwete kumpisha kwa muda kwenye kiti katika mkutano na Ma prezidaa wengine huko Yokohama ,Japan..

Nipo hapa jijini Yokohama, Japan. Nipo kwenye msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete kwenye mkutano mkubwa na maarufu duniani kuhusu Afrika unaojulikana kama TICAD V (Tokyo International Conference on African development). Kwa dakika chache jana Mhe. Rais Jakaya Kikwete aliniachia kiti chake, nikaa kwenye round table na marais wengine zaidi ya 50 wa nchi za Afrika! Can you imagine that? Kulia kwangu alikuwa Mhe. Michael Satta (Rais wa Zambia - a very charming fella!) na kushoto kwangu alikaa Mhe. Yoweri Museveni (Rais wa Uganda).

Leo tena nimepata fursa ya kuingia kwenye kikao kimoja na Mhe. Rais Jakaya Kikwete na humo tulikuwa kwenye bilateral meeting na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Mhe. Ban-Ki Moon. Pia nimepata fursa ya kujadili mambo kwenye vikao na Marais Jacob Zuma (South Africa), Ali Bongo Ondimba (Gabone); Rais wa World Bank, Dr. Jim Yong Kim; Rais wa Benki ya Afrika, Dr. Donald Kaberuka; Rais wa JICA, Dr. Akihiko Tanaka etc. Ziara hii imenifundisha mambo mengi ambayo sintoyasahau katika maisha yangu.

Nimepata pia fursa ya kumuelewa vizuri zaidi Rais wetu na namna anavyoielewa dunia, kukubalika kwake kimataifa, nafasi yake kati ya viongozi mashuhuri duniani na nafasi yetu kama Taifa katika dunia. Hongera Rais wetu Jakaya Kikwete, umenifanya nijisikie 'so proud to have you as our president, and to be a Tanzanian in a global world!' Ziara hii kwenye mkutano huu mkubwa wa kimataifa hapa Japan imenipanua zaidi uelewa wangu kuhusiana na diplomasia ya kimataifa na namna changamoto zinazotukabili sote kama raia wamoja wa dunia moja na namna zinavyopatiwa ufumbuzi wa pamoja, kwa namna ya umoja wetu kama binadamu.
 
So what?? Anyways

Happy birthday to him leo anatimiza 39yrs..kampita mwaka mmoja dida wa mchops..hahahah eti dida anajifanya 29 hahah
 
Kwani jk hakaimishi madaraka? Inawezekana vipi akaenda na urais Japan? Nadhani akisafili kuna mtu anashika nafasi hiyo na si mwingine ila ni makamu wa rais.
 
alikaa pale alipoamka jk tu wala hakukaimu chochote , ni kama ile ya january kula ugali na bush hotel moja ( siyo meza moja ) .
 
Alijifunza kumtelekeza baba yake mzazi,hadi masikini anatunzwa na kuhudumiwa na wasamalia wema.

nakuhakikishia kwamba laana hii haitamuacha salama huyu jamaa aisee , noma sana !
 
nakuhakikishia kwamba laana hii haitamuacha salama huyu jamaa aisee , noma sana !

Kumbe ana laana eeh? Ndio maana hata kule Bungeni anaongea mambo ya ajabuajabu. Unajua mkuu laana sio kuokota makopo tuu bali unajikuta unaongea ndivyo sivyo. Hivi hakuna wazee wakumshauri akamwangukie mzazi na kusamehewa? Ni ushauri tuu maana akisubiri MUNGU amchukue basi hiyo laana haifutiki.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Hivi kwa nini watu wanamuandama namna hii Kigwa? Anawatisha ama wanamuogopa?
 
Rais wa vitumbua atapita bila kupingwa ila wa Jamhuri laana ya mzee wake hata jina halitafikiriwa kubisha hodi NEC

Anachoripoti toka Japan sijajua ni ugonjwa gani kati ya yale
 
Back
Top Bottom