Kigali Rwanda

Kigali Rwanda

hazole1

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2015
Posts
4,319
Reaction score
3,919
fb5c64f8cb148f2f16eaeed914bf0e96.jpg
925083a9aff37766fe0e23eb2dabacc2.jpg
eeacbd0144e15c93d76f26a0c2ea10a9.jpg
2c661bcbeac895d677060317f35881a0.jpg
 
5c14a588318ca4ad28c4d873e193d0b4.jpg

Ni kutojua au kutotembea. Waliowahi kufika Sasolburg, kijimji kidogo sanaaa au tuseme ni kama kijiji huko Afrika ya Kusini, ndio tutajua nini cha kusifia au mifano ya kuiga na jinsi Mwafrika anavyotakiwa kujipanga kujikomboa, kulikomboa hili bara kwenye ujinga na umasikini.
Maendeleo sio majengo, na kazi za suti na tai. Kama majengo ni maendeleo basi Dubai ndio iwe mfano maana hakuna pazuri kama huko, kibiashara nk. Jangwa lilofanywa kuwa mji wa kisasa.
Sasolburg wanatengeza Mafuta yao wenyewe, Masuala yanayohusu gesi na rasilimali, hakuna cha mgeni hapo, akili ya wazawa na wamiliki ni wazawa, wafanyakazi wote niwazawa, Sasol ni Kampuni ya Kiafrika inayoshindana na Makampuni makubwa duniani kama Total, Shell nk. Teknolojia ya Mwafrika ya Kisasa katika kutoa nguvu za Umeme kupitia nguvu za Nyuklia.
Barabara za kisasa, vipato na mishahara mizuri, maisha bora, nyumba nzuri na mabwawa ya kuogelea, mashule na hospitali za kisasa, uwanja wa kucheza golf, mashamba yaliyostawi, mifugo pamoja na farasi mashambani. Watu sura zao ninaonekana zina furaha. Yanayotoka ardhini, yanawafadisha wazawa. Hamna Ubabe wala Ukandamizwaji wa kisiasa, hakuna lazima uwe chama fulani, au kuabudu au kuogopa wanasiasa. Huu ndio Urithi wa Utawala Bora wa akina Mandela na sera za chama tawala cha ANC.

Unajisikia sasa hivi ndio Mwafrika alitakiwa kuishi.
 
Neno mzawa unajua maana yake mkuu???

Maana hiyo South Africa ina wazawa weusi na weupe na hiyo kampuni unayoisema ebu jaribu kugoogle tena ..
 
Sisi Wamachinga wameruhusiwa na Rais kupanga bidhaa zao barabarani na kuchafua manadhari ya majiji na miji
 
mada zinakanganyikana humohumo ndo maana hata wakubw wetu wanazichanganya humuhumu
 
Ipo poa sana,nitaenda kupumzika siku inshaallah
 
Neno mzawa unajua maana yake mkuu???

Maana hiyo South Africa ina wazawa weusi na weupe na hiyo kampuni unayoisema ebu jaribu kugoogle tena ..

Tumekuelewa. Na swali lako ni zuri sana. Asante.
Katiba ya Afrika ya Kusini inasema hivi "Afrika ya Kusini ni ya watu wote wanaoishi".

Ni kweli neno au maana "Uzawa" limekuwa likizungumziwa sana.
Makaburu wanasema kuwa wao ni Wazawa pia. Maana hawajapishana sana na Uhamiaji wa kabila la Wazulu ambao ndio wengi kuliko wote. Wazulu pia ni Wahamiaji.

Na tukisema "Mzawa" katika Bara hili ni Mbantu tuu, Basi tutakosea maana kuanzia Equator kwenda juu, tabaka la Wabantu ni Wachache sana.

Afrika ya Kusini imejengwa na watu wote.
Makaburu hao waliishi hapo Afrika ya Kusini kama nyumbani kwao na waliijenga nchi hiyo kwa Uzalendo mkubwa. Waliwaona Waingereza kama Wakoloni, na waliwapinga, walipigana nao na walipandisha bendera ya Uhuru. Hawakuweka mguu mmoja ndani, na mmoja nje. Na hata baada ya kuwapa Waafrika Uhuru wao, bado Makaburu wameendelea kuisaidiana Serikali kujenga nchi yao.
Saa nyingine Makaburu wanaonyesha Uzalendo wa hili bara zaidi ya wewe na mimi.
Makaburu hawakutorosha mali na kwenda kujenga Ulaya au sehemu nyingine duaniani.

Walichokosea ni Imani zao potofu kuwa Mwenyezi Mungu aliwapa Afrika kama zawadi, na Mwafrika amezaliwa kumtumikia Mtu mweupe mpaka siku ya Kiama. Ndio maana Makaburu walishirikiana na Israel ya Kizayuni kwa sababu wote wanatawala kwa misingi hiyo hiyo ya Ubaguzi.

Serikali ya Waafrika imejitahidi kurudisha Usawa katika Uchumi kwa kuwapa Waafrika au watu weusi nafasi na wao pia wafaidike. Na kwa kipindi cha miaka 22 sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa sana kwenye kipato cha Mwafrika.

Chama Tawala cha AnC walikuwa na uwezo wa kuwanyang'anya na kutaifisha mali zote kutoka kwenye mikono ya Wazungu wachache. Lakini walijiuliza, je Waafrika wana uwezo huo wa kuendeleza safari hiyo?

Walichukulia mifano katika nchi za Kiafrika waliorithi mazuri kutoka kwa Wakoloni na kuishia kwenye uharibifu tuu.
Uchumi haukuguswa bali ulipanuliwa, na Wazungu na kipaji chao pia walitunukiwa na waliombwa kuwaelimisha Waafrika ambao waliwekwa kwenye giza zaidi ya miaka 400.

Hospitali kubwa kuliko yote duniani, inasemekana iko huko Soweto inaitwa Chris Hani Hospital au Baragwana na ilijengwa na Serikali ya Makaburu na inayoa huduma sisi tunayoifuatia huko India.

Kuinua hadhi ya Mwafrika na kumkomboa kwenye Umasikini, Ubinaadamu ndio imekuwa dini ya Chama Tawala cha ANC.
Sheria za kazi Afrika ya Kusini lazima watu 7 wawe Waafrika, mmoja Mzungu, mmoja Mwindi na moja awe Chotara. Waafrika wamepewa kipa Umbele. Na Waafrika wanasukumwa kwenye nafasi za juu.

Na Mabenki kutoa mikopo, kuzadiwa Tenda za Serikali, kupewa nafasi za biashara, zinapewa kipaumbele kampuni zilizokuwa na Wafanyakazi wengi walio Watu Weusi.

Hatuangalii kwenye Google, tumeshafika Rwanda, na tumeshafika Sasolburg.

Kama wewe ni mtu wa Gugo, Naomba pia uangalie Mossey Bay. Hii ni miji midogo sana ambayo imeishinda miji au nchi nyingi za Afrika kwa maendeleo, na mifano ya kuiga lakini watu wamenyamza, wamefanya vitu vyao. Binaadamu ana uwezo mkubwa sana.
 
5c14a588318ca4ad28c4d873e193d0b4.jpg

Ni kutojua au kutotembea. Waliowahi kufika Sasolburg, kijimji kidogo sanaaa au tuseme ni kama kijiji huko Afrika ya Kusini, ndio tutajua nini cha kusifia au mifano ya kuiga na jinsi Mwafrika anavyotakiwa kujipanga kujikomboa, kulikomboa hili bara kwenye ujinga na umasikini.
Maendeleo sio majengo, na kazi za suti na tai. Kama majengo ni maendeleo basi Dubai ndio iwe mfano maana hakuna pazuri kama huko, kibiashara nk. Jangwa lilofanywa kuwa mji wa kisasa.
Sasolburg wanatengeza Mafuta yao wenyewe, Masuala yanayohusu gesi na rasilimali, hakuna cha mgeni hapo, akili ya wazawa na wamiliki ni wazawa, wafanyakazi wote niwazawa, Sasol ni Kampuni ya Kiafrika inayoshindana na Makampuni makubwa duniani kama Total, Shell nk. Teknolojia ya Mwafrika ya Kisasa katika kutoa nguvu za Umeme kupitia nguvu za Nyuklia.
Barabara za kisasa, vipato na mishahara mizuri, maisha bora, nyumba nzuri na mabwawa ya kuogelea, mashule na hospitali za kisasa, uwanja wa kucheza golf, mashamba yaliyostawi, mifugo pamoja na farasi mashambani. Watu sura zao ninaonekana zina furaha. Yanayotoka ardhini, yanawafadisha wazawa. Hamna Ubabe wala Ukandamizwaji wa kisiasa, hakuna lazima uwe chama fulani, au kuabudu au kuogopa wanasiasa. Huu ndio Urithi wa Utawala Bora wa akina Mandela na sera za chama tawala cha ANC.

Unajisikia sasa hivi ndio Mwafrika alitakiwa kuishi.
Na yenyewe ni Africa mashariki?
 
Maendeleo sio picha za majengo, hata ukiletewa picha za Dar sehemu nzuri nzuri unaweza ukasema watu wanaishi kwa raha, kumbe Shetani baba kawageuza Masetani wana, maendeleo ni mchanganyiko wa mambo tofauti zikiwemo huduma bora za jamii sio bora huduma n.k
 
Back
Top Bottom