Kifo cha mende kinainyemelea CUF Zanzibar kwa kasi

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,790
Katika hali isiokuwa ya kawaida na baada ya chama cha CUF kikizidi kudhoofika kiitikadi na mshikamano, Viongozi wa juu wa chama hicho wamekuja na mbinu mpya ya kutoa upinzani nje ya Baraza ja Wawakilishi kwa kutoa "ma-Tamko" ya kupinga na kukosoa kwa kila linalofanywa na serikali ya CCM . Tamko la juzi la CUF ni kuhusu jinsi hatua za SMZ inayozichukua kukabiliana na kipindupindu, bila ya kutoa njia mbadala au ufumbuzi .

Ni kweli usio shaka kuwa mshikamano wa viongozi wa CUF bado ni mkubwa na wenye nguvu, lakini hofu iliotanda ndani ya chama kama wataweza kuudumisha mshikamano huo kwa muda wote hasa kwa wanachama na wapenzi wa kawaida.

CCM katika kujibu matamko hayo kwa njia za ishtizai na dharau wamekuja na kauli mbiyu " Uchaguzi umekwisha, sasa ni wakati wa matayarisho ya uchaguzi 2020" Kauli mbiyu hii imewafanya wana CUF wengi kupoteza "ungangari" kwa kuchoshwa na kauli za viongozi wao zisiokuwa na mashiko wala mantiki zilizobatizwa jina la "Drip". Drip ni neno la vijiweni la kupeana habari za kisiasa za matumaini yasiokuwepo kuwa CUF itapewa madaraka yake hivi karibuni.

Kuna kila ishara kuwa " kifo cha mende" kilichotabiriwa na Babu Juma Duni kimepiga " U Turn" na kuelekeza miguu kwa chama CUF. Kosa waliolifanya kususia uchaguzi sasa linawaandama na kuigharimu CUF na Zanzibar kwa ujumla. CUF ikiri kuwa Maalim Seif sasa amegonga ukuta , kifikra, kisiasa na kimkakati.
 
Back
Top Bottom