Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,209
- 4,406
1)enyi makampuni simu,mbona lugha mwachafua.
Kusema yanilazimu,lugha yenu nachukia.
Kiswahili si kigumu,vipi mnakibomoa.
Tena mnakipa sumu,kife huku chakodoa.
Ningewa kifimbo cheza,bakora ningetembeza.
2)kwenye wenu usahili,kingereza haribika.
Mwaona ujahili,wala tujaelimika.
Vipi hiki kiswahili,mnataka kukizika.
Hivi kweli mnajali,kwamba sisi twaudhika.

3)kama lugha hamjui,simuwafate wajuzi.
Ama hamkitambui,kiswahili si cha juzi.
Utakipata shelui,hata kwenye king'amuzi.
Kama nyinyo hamjui,vipi yu mchunga mbuzi.

4)matangazo redioni,lugha mwaivunja vunja.
Nu mbaya masikioni,mbona mwaikunja kunja.
Kwa zawadi za dukani,mbovu mwapigia mbinja.
Yakera masikioni,lugha mnavyoipunja.
Ningewa kufimbo cheza,bakora ningetembeza.
5)msijifanye vipofu,katika lugha za watu.
Lugha mwaitia hofu,tena mwazidisha kutu.
Hiyo si nyama ya pofu,muipake ukututu.
Msiifanye nyamafu,ije nuka kama kutu.

Shairi:KIFIMBO CHEZA.
mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0655519736.