Naombeni kufahamishwa kuhusiana na kifimbo kile cha mwalimu Nyerere. Alikipata wapi, na je habari zilizoenea huku mtaani kuwa eti aliwahi kukisahau hotelini wakati akiwa ziarani ulaya, lakini wahudumu wa hoteli walishindwa kukitoa juu ya meza ni za kweli?
Kipo wapi kwa sasa?? Makumbusho au alizikwa nacho??
Kuna stori nyingi tu mtaani kuhusu kile kifimbo, na nyingi huwa ni hisia tu za watu....hata mm nlisika alikipata kwa mganga maarufu akiwa na kenyatta enzi hizo
nakumbuka walisema mama yake ndie ngao yake na mlinzi wake mkuu wakasema
mama yake akifa hataishi miaka miwili wkt huo nikiwa mkwawa high school
sikuamini hayo ila alipofariki ndani ya miaka 2 tangu afe mama yeke nkaanza kupata mashaka na yaliyosemwa juu yake
kile kifimbo wadau walisema pia haendi nacho kanisani hata kidogo sina uhakika kwa hili.
Kama unayo yasema ni kweli basi alikuwa mchawi au anatumia majini.
Ukienda pale mwenge wanapochonga vinyago utavipata,Kumbe kuwa na kifimbo ni heshima?? Alikipata wapi?
Asante sana, nitaenda kutembelea huko makumbusho Butiamawakati anapigania uhuru alipenda kutembea na bakola.baada ya uhuru akawa anatembea na fimbo ndogo zaidi ya ile ya uhuru kwa urefu.baada ya kustaafu alikua na fimbo nyingine iliyotengenezwa kwa pembe ya ndovu kwa kila ncha lakini katikati mti.fimbo zote zipo butihama kwenye jumba la makumbusho la nyerere lililojengwa miezi saba kabla ya kifo chake.roger
Kitavi mpaka miaka ya leo unaamini uchawi?Hawezi kuthibitisha!
Yalikuwa mazungumzo baada ya habari na shabban kisu au tumbo risasi....