Kifahamu kikosi hatari duniani cha u.S.A navy 'seal' tayari chatua rasmi rasi ya North Korea

Eddy Love

JF-Expert Member
Jul 25, 2011
13,654
8,561
KIKOSI HATARI CHA US NAVY 'SEAL' CHATUA RASMI RASI YA NORTH KOREA

Yumkini jaribio la mzee wa kiduku limeshtua sana Marekani ambapo sasa ni rasmi Kikosi hatari cha Makomandoo wa Kimarekani ambacho ndicho "The Most Feared Force" katika ulimwengu huu cha US NAVY SEAL inasemekana tayari kiko katika Peninsula ya Korea tangu Jana usiku kikitokea jimbo la Florida nchini Marekani.

Hiki ni kikosi hatari zaidi duniani ambacho kazi yake ni kufanya operations ambazo ni hatari zaidi mno na za mwisho. US Navy Seal ni mjumuisho wa makomandoo hatari zaidi wanaotumia ujuzi wa hali ya juu na wenye mafunzo ya kitaalamu zaidi kuliko makomandoo wengine wa majeshi yote ya kimarekani.

Makomandoo hawa ni wale tu wenye uzoefu wa hali ya juu wa kupambana popote pale iwe angani, ardhini au majini, na katika hali yoyote ile iwe barafu, mvua au jua. Na ndio maana ya neno SEAL ambayo kirefu chake ni Sea, Air and Land.

Ni Mara chache sana kutumika. Hawa ni tofauti na majeshi mengine kama US Army Rangers, US Delta Force na mengine. Katika utawala wa Obama, ametoa ruhusa MARA MOJA tu kwa US Navy Seal kutumika. Mara ya mwisho kilitumika usiku wa manane kwa takribani dakika 45 tu kumuangamiza Osama na ni askari mmoja tu alijeruhiwa kwa ajali ya helkopta zisizotoa sauti ambayo ilikosewa ikagonga ukuta wakati makomandoo wakidrop kwenye makazi ya Osama.

Na baada ya Operation Makomandoo hao waliilipua haraka helicopter yao iliyopata hitilafu ili maadui wasigundue teknolojia iliyotumika kutengenezea helicopter hiyo na baada ya kuilipua wakaondoka. Makomandoo wa Navy Seal waliotumika katika Operation hiyo ni 11 tu na Marubani Watatu ambao nao ni kutoka Navy Seal. Na ikumbukwe kuwa Operation hii ilikuwa ikitazamwa live (mubashara) kutoka White House ambapo Obama alikuwa akifuatilia (nilirusha tukio hili), kofia za makomandoo hawa zilikuwa na kamera mbele ambazo zilitumika kurekodi kila kitu kinachoonekana mbele na kurusha kwenye satelaiti had White House. Mkakati huu ulisimamiwa na Mwanamke hatari zaidi anayejulikana kama Alfreda Frances Bikosky ambaye ni Afisa mwandamizi wa CIA na jasusi aliyebobea na pia ni komandoo lakini si memba wa Navy Seal. Bibi Alfreda anajulikana zaidi katika jeshi la Marekani kama MALKIA WA MATESO. Serikali ya Marekani inajitahidi kudhibiti mitandao ya kijamii na google isisambaze picha za mama huyu hatari.

Kikosi hiki cha US Navy Seal hutumika baada ya makomandoo wengine wa majeshi tofauti ya marekani kusoma Jiografia ya sehem husika, ramani ya ngome za adui na silaha zake then Raisi wa Marekani hutoa ruhusa ya NAVY SEAL kutumika kumalizia Operation. Baadhi ya majukumu/kazi za Navy Seal ni Direct Operations (kama wanavyotaka kumfanyia North Korea), Strategic Special Missions (kama walivyofanya kwa Osama), Hostage Rescue (kama walivyofanya miaka ya nyuma kuwaokoa Ma-Intelligensia wa Kimarekani waliotekwa Iran) na Foreign Internal Defence.

Mpaka sasa Navy Seal ina jumla ya Makomandoo 8985 ambao ni hatari mno na wenye roho za kinyama. Makomandoo hawa huwa wapo kwenye mazoezi makali ya special operations na trainings ngumu muda wote huko Virginia, Marekani. Mara chache sana Navy Seal huwa Recruited kwenda CIA kufanya kazi za Kiintelligensia wanapotakiwa. Makamu wa Rais wa Marekani Bwana Pence yuko Korea Kusini na inasadikika ujio wake umeambatana na NAVY SEAL waliojichimbia katika Nyambizi zisizoonekana katika pwani ya Korea..
 
Endeleeni kujidanganya na Movie za The Expandeble Hii Ngoma Ya Kweli Sio Maigizo ,Kama Vietnam iliwatoa Nishai Tambueni Aibu ya Karne inakuja Soon Mnavyojidanganya kuwa Mnyoa kiduku Haijui Marekani akurupuke tu Wewe uliye hapa JF Ndio unajuwa vizuri
 
Mmmh. sio kwa mwanamama huyo. Bora tu wafiche sura yake,lakini kwanini wanapenda kutishiana na kutaka Vita?? Halafu miTz mlivyo mamburula wengine mnashadadia kabisa,hivi mnajua Hzo nchi kina wanwake kama wanawake zenu,kuna watoto kama watoto wenu,kina wazee kama wazazi na wazee wenu babu na bibi??? Acheni jamani kushangilia Haya matukio
 
umeiongelea marekani kwa mbwembwe..he Korea Na makomandoo wao. intelligence yao unaijua???

Kwa akili zenu mnadhani North Korea Hana espionage? Hayajui hayo...he marekani Kama anafanya hivyo Mapanki hatapata hasira Na kurusha kitu kakaenda tua ndani ya US? he unajua wao hawana enter continental missile?
 
Mmmh. sio kwa mwanamama huyo. Bora tu wafiche sura yake,lakini kwanini wanapenda kutishiana na kutaka Vita?? Halafu miTz mlivyo mamburula wengine mnashadadia kabisa,hivi mnajua Hzo nchi kina wanwake kama wanawake zenu,kuna watoto kama watoto wenu,kina wazee kama wazazi na wazee wenu babu na bibi??? Acheni jamani kushangilia Haya matukio
Mi Tz ndio nini uwe na adabu we mama nata mani kukutukana una jua maana ya Mi Tz mamaeeee uwena adabu alafu
 
Wanachotaka Ni Kujilinda, Unatoka Maili Maelfu halafu ati Unasema wao ndio wachokozi!



KwaKujifunza siasa za Dunia Nimegundua, Matatizo ya Kiusalama Duniani yanasababishwa na Mataifa Malaya, yasiyoweza Kutaka Kuona Majirani zao wakiwa na Nguvu za Kijeshi, Hivyo Mataifa hayo yanaenda Kuita amajeshi ya Nchi Kubwa maelfu ya Maili na Kuwarubuni kila siku wamdhoofishe Jirani Yao!

Pia Nimejifunza Nchi Zinazosema ati zinavamia Nchi nyingine kwa Kuwa ni Tisho kwao sio Kweli, Nchi hizo hazijaribu hata Kidogo Kuzivamia au Kuzichokoza zile Nchi zilizotishio Kweli. Huwezi Ukawa Una Mizinga ya Nukilia 20,000 na Madege na Manuari mamia kwa mia halafu eti Unahofu nchi yenye tubumu tutano!

Shida sio Kuihofu? Shida ni Kuwa, Nchi ikishakuwa na Nyukilia na Uwezo wa Ku-deliver basi wewe na hizo nchi Malaya zako unakuwa Umepoteza Uwezo wa Kuwatawala, Kuwaburuta na Kuwapangia Maisha. Kwa hiyo Hizo nchi zinaonekana Ni tishio sio kwa Kuwa Sitakuvamia, Bali utapoteza Uwezo wa kuwatawala na Kuwapangia Maswala. Huo ndio Ukweli.

Nyukilia Ni kama Channjo ya Kufanyiwa Agressions. Nchi zinazotafuta sana Kuwa na silaha za Nyukilia sio kweli zinatafuta kuzitumia kuvamia Mataifa Makubwa bali wanataka ziwe Ni Vaccine kwa Usalama wao Kwi sijawahi ona Nchi yenye Nyukilia Ikavamiwa na Nchi nyingine Tangu Kumalizika kwa WWII.
 
Marekani Wanaweza Mwishoni Wakaipiga North Korea tena Kipigo. Lakini North Korea Marekani Itaweza Tu Kuwapiga bila Kusababisha Madhara kwa South Korea Iwapo Watawalenga na Makombora ya ICBM kama 100 hivi na kuua kila mtu kwa mpigo mmoja! Kufanya Hivyo Kwa watu ambao hawajakuchokoza Utakuwa ni Adui wa Dunia Nzima Na kuna consequences zake mbaya.

Iwapo Marekani wakiipiga NK kwa Kudonoa, Pigo la Kwanza tu North Korea wataipiga South Korea kwa kila walichonacho, Nuclea etc. Na ni habari ya Uhakika NK wana Mizinga ya Roketi zaidi ya 10,000 Zimeelekezwa Seol, Hii tu ukiacha Nyukilia inatosha Kufanya Mji wa Seol Kuwa Majivu in one day!

Swala la Kujiuliza, Is this Really necessary? Maana it is For sure North Korea wakishambuliwa na mzinga mmoja tu ndilo watakalolifanya. Hawatarisk kusubiri, na Dunia itawaelewa kwani wamechokozwa!

 
Marekani hutushia vijinchi vyetu vya Afrika na Mashariki ya kati ijaribu North Korea ione. North Korea ni nchi bhana acha viji nchi vyetu ivi ambavyo vimedumazwa na Marekani.
 
Hawa wanattunishiana tu misuli nguvu zote walizonazo wanaogopana maana NK anajua wapi pa kupiga akishambuliwa na US kwa maana hiyo SKhawezi kukubali US wapigane na ndugu zao maana wanajua hasira zote zitawamaliza wao
 
Back
Top Bottom