Kidumu Chama Cha Mapinduzi

Kidumu Chama Cha Mapinduzi

Joined
Jul 24, 2013
Posts
32
Reaction score
8
Chama Cha Mapinduzi siku zote ni chama makini kinachoendeshwa kwa misingi ya kanuni na taratibu bila ubabe. Kwa miaka iliyopita chama hiki kikongwe kilionekana kufa kumbe kilikuwa kinajitathimini upya na kujisahihisha upya.

Kutokana na kasi hii ya Rais Magufuli ni imani yangu kuwa CCM kitaendelea kuongozwa dola kwani ni chama pekee barani Afrika kinachokubali kujikosoa na kujisahihisha na kisha kuendana na siasa za ushindani na sio siasa za mazoea. Bado ni chama makini na mimi ni mtu makini.

Hongera CCM yangu.
 
Chama cha mapinduzi siku zote ni chama makini kinachoendeshwa kwa misingi ya kanuni na taratibu pasi bila ubabe, kwa miaka iliyopita chama hiki kikongwe kilionekana kufa kumbe kilikuwa kinajitathmini upya na kujisahihisha upya. Kutokana na kasi hii ya Rais Magufuli ni imani yangu kuwa CCM kitaendelea kuongozwa dola kwani ni chama pekee barani Afrika kinachokubali kujikosoa na kujisahihisha na kisha kuendana na siasa za ushindani na sio siasa za mazoea. Bado ni chama makini na mimi ni mtu makini.

Hongera CCM yangu
 
Magufuli kashasema yeye sio mwanaccm... hata kwenye kampeni hakuwa anaitaja ccm... anajua ccm imeoza umebaki kutupwa jalalani
 
Pamoja na mapungufu yaliyo ndani ya CCM, wananchi wa Tanzania tunalazimika kukimbilia huko kwa kuwa wapinzani wametusaliti. Haiingii akilini, miaka zaidi ya ishirini, upinzani hawana hata mtu mwenye sifa ya kugombea uraisi hadi wamsimamishe aliyekataliwa na CCM tena kwa kashfa. Cha kusikitisha ni kwamba, si tu aliyesimamishwa kwa ticket ya UKAWA alikuwa ni mtuhumiwa namba moja wa wizi serikalini (kwa mujibu wa CHADEMA), pia hata uteuaji wake kugombea uraisi haukufuata utaratibu wa kidemokrasia, kitu ambacho kiliwaacha Watanzania wengi midomo wazi wakijiuliza "inakuwaje mtu anajiunga leo na chama, halafu kesho yake anagombea uraisi". Kwa mwendo huu, hatuna budi kuwaunga mkono CCM maana walau wana utaratibu ambao usipofuatwa, unaweza kwenda mahali na kuulalamikia, ndani ya chama. Lazima tukubali ukweli, wapinzani wanafanya mambo kiholela na hili ni tatizo kubwa saana kwa taifa. Leo hii wapinzani walichonacho hata hakina jina, maana UKAWA walianza kama mwamvuli wa kupigania Katiba ya wananchi, lakini kwa sasa hata sijui wanachofanya ni nini. Labda wewe mpinzani tusaidie.
 
Simba bila yanga mpira utakufa tz. Ukiritimba wa kisiasa wa ccm lazima utokomezwe ndio wananchi tutapata maendeleo ya kweli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom