Kidedea wa Al Ahly Hawa Hapa

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,258

Mashabiki maarufu wa Al Ahly ya Misri, Ultras Ahlawy wako jijini Dar es Salaam na wamekuwa wakifanya vurugu ile mbaya katika eneo la katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Mashabiki hao ambao wengi wao ni vijana, wamefikia Kariakoo jijini Dar es Salaam, kila jioni waaanza “amsha amsha” si mchezo.
Kuonyesha kuwa Ultras Ahlawy wako makini na kazi yao, leo wameenda kupiga mazoezi ya ushangiliaji kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wakati timu yao inafanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja huo, wao walikuwa wakipiga tizi la kushangilia utafikiri mechi.

Yanga itakuwa kazini kwenye Uwanja wa Taifa, kesho kuwavaa Al Ahly katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayosubiriwa kwa hamu kuu.
 
Bila ya unafiki, najiandaa kwenda taifa na jezi zangu za Simba kuwacheki wa kimataifa, sitakaa mbali na hao mashabiki wa Al Ahly.
 
Sina urafiki na yangu na kama uzalendo unapimwa kwa kulamishana kuishangilia team usiyoipenda wacha mie nisiwe mzalendo na ninaombea yanga wabugizwe magoli double double
 
Uzalendo kwanza hao ni wa kupuuzwa tu na pua zao ndefu.

Bora nishangilie paka na paka " wakitinduana " kwa kufanya " mapenzi " kuliko kuniambia niishangilie Yanga. Bora ya shetani kuliko Yanga. Al Ahly leta heshima na utulivu leo hapa jijini ili tuheshimiane na nipigie hao vyura fc goli nne ( 4 ) tu kisha warudi wakajipange kuitisha uchaguzi klabuni kwao.
 
Kila Simba atakiri kuwa Yanga ni bwana.....!!!

Nyau fc karibuni kwenye episode nyingine ya "kampa kampa tena!!!"
 
Kwa hiyo leo tutegemee kuwashuhudia waarabu weusi uwanja wa taifa wakiipa nguvu timu yao! makubwa haya!!
 
Back
Top Bottom