kuna jamaa wanajiita laser unicorn wali kickstart project yao inaitwa kung fury na walichangiwa zaidi ya $600,000 (zaidi ya 1.2 bilioni za kitanzania) moja ya matokeo yake ni movie yao fupi ya dakika 30.
movie hii ya kung fury wame act kama miaka ya 1980's ni action comedy, nimeangalia dakika zote 30 wajamaa wamejitahidi sana movie ni nzuri na huwezi kuamini kama imetengenezwa kienyeji. jambazi hitler aka kung fuhrer, kuwa master wa kung fu kwa chini ya sekunde moja na mambo mengi yapo humu.
icheki hapa kihalali maana kuna watu hawajawahi angalia movie isiokuwa ya piracy
https://www.youtube.com/watch?v=bS5P_LAqiVg
producer/designer/animator wa kibongo tunaweza hii?