Kibu analeta sanaa ya mpira kama walifanya wakina Fei na Dube, Simba wajiandae kwa lolote

Aug 29, 2022
84
175
Kibu analeta sanaa ya mpira kama walifanya wakina Fei na Dube, Simba wajiandae kwa lolote
Kiungo mshambuliaji wa Simba sc Kibu Densi amegoma kusaini mkataba mpya akiwa ameweka vikwazo vingi kwa viongozi wa Simba.

Na inavyoonesha Kibu aonekana ana ofa kubwa zaidi nje ya mipaka ya Tanzania kwahiyo ameanza kushinikizwa na wanao msimamia na yeye mwenyewe ameonyesha nia ya kutoendelea kucheza Simba.

Sasa ukilitazama hili suala binafsi bado naona kuna sanaa inayoendelea kwa wachezaji wengi baada ya kupata jina kubwa na kuibwa ndani ya klabu yake yaani kuonesha kuwa ni muhimu kwahiyo inapelekea kutumia fursa ya kupiga hela ndefu.

Lakini kwa ushauri wangu tu hizi sanaa ni mbaya kama mchezaji aliyekuwa kama anahisi anahitaji kwenda kucheza mpira sehemu nyingi aende kwa mazungumzo mazuri na viongozi kuliko kufanya vituko kama anavyovifanya Kibu au Feisal na Dube.
 
Huyu anawaseti mjae kama kipindi kile Cha zimbwe alivyowaseti anagombaniwa na club za south, mkampa mkataba mkubwa, ndo anachofanya kibu

Hebu nitajie timu yenye hadhi ya Simba ambao wanaweza mchukua kibu akaingia kwenye kikosi Chao?


Alafu acha kumfananisha kibu na callibre za kina fei na dube sawa??


Huyu kibu tangu msimu uanze kafunga goli Moja tena kwenye mechi ya 5-1...
 
Yaani mashaabiki na wadau wa kabumbu wana ULEMAVU WA KUFIKIRIA.
Yaani mchezaji KUJITHAMINI na kutambua ubora wake ili alipwe lingana na thamani yake eti wao wanaita ni USANII!
 
Feisal alishatengeneza hiyo desturi, na upande wa pili mlishangilia, sasa msumeno unaitikia kwenu. Tuvumilie tu!
Ndio madhara ya kuingiza siasa kwenye mpira.
 
Kibu nae ana majukumu,mpira ni kazi mwacheni
 
Simba ifumuliwe yote waondoke wote wabaki wale wafia timu tuu wanaojulikana kina zimbwe..
Mtani wangu unatakiwa utambue kuwa mpira wa sasa ni uwekezaji! Na ninaposema hivyo, namaanisha pesa! Siku hizi hakuna tena mambo ya kufia timu.

Wekeni mzigo wa kutosha mezani, ili kijana asaini mkataba mpya. Kinyume na hapo, mhesabie maumivu.
 
Kweli malipo no hapahapa, mlivyoshangilia kwa fei mlidhani hayatawakuta..?
Kibu apige hapo hapo kwenye mshono
 
Sasa kibu si wamuachie haraka sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…