Kibonde wa Clouds acha kubeza kasi ya Mh. Rais na Serikali yake

sem2708

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,410
4,529
Nimeshangazwa na u-turn ya baadhi ya watangazaji wa clouds kwa jinsi wanavyobeza utendaji wa serikali ya tano. Mfano leo katika kipindi cha jahazi ,kibonde wa clouds anabeza utumbuaji wa majibu,eti kila kukicha ni fukuza fukuza.

Binafsi nimechukizwa sana na kauli hii na nina jiuliza ni nini hasa dhamira ya mtangazaji huyu.
Tumekuwa tukichukizwa sana na ufisadi na uzembe serikalini,iweje leo tumempata rais mwenye dhamira ya dhati ya kushughulikia majipu halafu atokeze mtu kwa kutumia jukwaa kubwa kama clouds abeze juhudi hizo?

Naamini wengi wa wanaolalamika aidha ni mawakala wa majipu au ni wanufaika na wametega mirija yao wananyonya kifisadi, sasa mimi nasema RAIS ENDELEA MBELE KWA MBELE asilimia kubwa sana naweza sema 99% ya watz ndio mambo tulikuwa tunatamani kuona nidhamu na weledi serikalini....
 
Hao wameadhirika sana awamu hii na vile vile mtu wao JM ndoto zake zinafifia kila kukicha.
 
Kama hupendi funga redio.

Tanzania si ina uhuru wa vyombo vya habari?

What's next? Utakemea wanaochora vikatuni vya Magufuli ?
 
No upambe anymore.

Hawa wamekalia mipasho na umbea ndiyo kula yao inaingia
 
Mkuu tunachoshangaa ni kuhusu kubadilika kwa watangazaji.

Zamani walikuwa wanasifu kila kitu hadi vitu vya kijinga.

Leo wanaponda kila kitu hadi kinachotakiwa kusifiwa.
Utawaamuliaje kipi kinafaa kisifiwa na kipi kinafaa kupondwa?
 
I really wonder what happened, at this time ingekuwa ni busara kusoma upepo maana watz wengi wanapenda sana mnyoosho huu wa JPM. Sasa watu wanashangaa heee,huyu vipi? anataka nini sasa ?
 
Umesema wanaponda kila kitu hadi kinachofaa kusifiwa.

Wewe ni nani uwaamulie wao nini kinafaa kupondwa na nini kinafaa kusifiwa?

Mkuu unapotoa maoni unabase upande wako, kile ambacho wewe unasifu unaona kama kila mtu alitakiwa asifu hicho.

Na vivyo hivyo kwa kile unachokiponda, so mimi kutamka vile siyo amri wala sheria, ni maoni yangu tu.

Halafu kuna vitu vinakuwa obvious kila mtu anasifu, halafu mtu anaibuka anaponda, lazima tumshangae.
 
Back
Top Bottom