KIAPO: Ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma na sekta binafsi

Cicadulina

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
977
2,369
Masharti ambayo mtumishi wa umma atatakiwa kukiri na kusaini ifikapo tarehe 15/01/2016 ni pamoja na
  1. Nitakuwa Mzalendo kwa nchi yangu na mtii kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  2. Nitahudumia umma na watumishi wenzangu kwa heshima
  3. Nitatimiza wajibu wangu kwa kutoa huduma bora kwa umma
  4. Nitatoa huduma bora kwa usawa kwa watu wote na kutofanya ubaguzi kwa misingi ya dini, siasa, kabila, udugu, ukanda, jinsia, urafiki au hali ya mtu
  5. Sitatoa, kushawishi, kutoa wala kupokea rushwa
  6. Sitaomba, kutoa wala kupokea zawadi au fadhila za kiuchumi au za kisiasa au kijamii zisizoruhusiwa na Sheria
  7. Sitatumia madaraka yangu kwa manufaa binafsi ya undugu, urafiki au jamaa zangu
  8. Nitatekeleza wajibu wangu kwa kufuata sera, sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali ya utumishi wa umma
  9. Nitafanya kazi kwa bidii na nidhamu ya hali ya juu
  10. Nitalinda na kutumia rasilimali za umma kwa manufaa ya umma
  11. Nitaepuka tabia ambayo inavunja heshima ya utumishi wa umma hata ninapokuwa nje ya mahali pa kazi
  12. Sitatoa siri za serikali au za mteja kwa watu wasiohusika isipokuwa kwa maslahi ya umma
  13. Nitajiepusha na mgongano wa maslahi na pale utakapojitokeza nitautatua kwa maslahi ya umma.
Aidha, vigogo wamebanwa zaidi pia kupitia kiapo chao chenye masharti 12, baadhi yakiwa ni “Sitatumia cheo changu au wadhifa wangu kwa maslahi binafsi, ya familia yangu, ndugu zangu au marafiki zangu isipokuwa kwa maslahi ya umma; Sitaomba, kushawishi, kutoa wala kupokea rushwa.

Vilevile, sehemu ya masharti 14 kwa sekta binafsi yanaeleza kuwa “Hatutashawishi, kuomba, kupokea au kutoa hongo au aina yoyote ile ya Rushwa; Hatutatoa, kuwezesha, kushawishi au kutoa zawadi kwa afisa yoyote wa umma familia zao au washirika wao wa kikazi katika shughuli inayohusiana na mchakato wa manunuzi au katika utekelezaji wa mkataba.
 
Last edited:
Back
Top Bottom