Kesi ya Mhindi ‘muuaji’ yazidi kukwama

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,181
Reaction score
166,164
KESI ya mauaji ya mfanyabiashara Abdulbasiti Abdallah (21), yanayodaiwa kufanywa na mfanyabiashara wenye asili ya kiasia Vinoth Praven (23), imeahirishwa hadi Februari 9, mwaka huu.

Mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Devota Kisoka imedaiwa kuwa kesi hiyo imeahirishwa kwakuwa jalada la kesi hiyo bado lipo kwa Mwendesha Mashitaka wa Serikali.

Mshitakiwa Praven anakabiliwa na kesi ya mauaji ambapo mpaka sasa anaendelea kusota rumande.

Mshitakiwa Praven anadaiwa kuwa Februari 6 mwaka jana, alimuua rafiki yake, Abdallah.

Awali mshitakiwa Praven alinaswa akiwa na mke wake Komal Katakia Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere wakijiandaa kutoroka baada ya mauaji hayo.

Hata hivyo upande wa mashitaka ulimuachia mke wa mshitakiwa huyo na kudai kuwa hawaoni sababu za kuendelea kumshtaki kutokana na makosa yaliyopo mbele ya mahakama.

Kesi hiyo itatajwa tena Februari 9, mwaka huu.
 
Hivi siku za nyuma kuna wahindi fulani waliua mfanyakazi wao aliyekuwa anajua mchezo wao wa kukwepa kodi na wakaenda kumtupa kule barabara iendayo Bagamoyo, kesi yao iliisha vipi? anayejua naomba msaada!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…