choga mkuu
JF-Expert Member
- Apr 11, 2016
- 283
- 110
MAHAKAMA YA MKOA MOROGORO YA MWACHIA HURU,MEYA KINONDONI NA WENZAKE 10
Leo siku ya jumanne ya tarehe 03 May 2016, muda huu (saa Nne asubuhi) ,mahakama ya mkoa Morogoro,imemwachia huru Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Boniface Jacob na wenzake 10, katika kesi namba 156 ya mwaka 2015,iliyokuwa inawakabili juu ya mkusanyiko usiohalali"unlawful assembly" iliyokuwa ikisikilizwa mkoani Morogororo,mbele ya Mheshimiwa Hakimu ERIC RWEHUMBIZA.
Aidha kufutwa kwa kesi hii namba 156 ya mwaka 2015,ni kutafanya watuhumiwa kuwa huru,baada ya kufutwa pia kesi namba 157 ya mwaka 2015 mahakama ya mkoa Morogoro,ilikuwa pia inamkabili Mhe. Boniface Jacob kwa shitaka la kuendesha mafunzo ya "RED BRIGADE" katika wilaya ya Mvomero na Morogoro mjini.
Kufutwa kwa kesi zote mbili 156 na 157, kumelete shangwe na furaha katika viwanja vya mahakama ya mkoa Morogoro.
Mstahiki Meya wa Kinondoni Mhe.Boniface Jacob yupo njiani kurejea Dar es salaam,kwa majukumu yake ya kawaida.
Kutoka Mahakamani-Morogoro
Chadema Media