Kesi ya kupinga ubunge Igunga leo

Aisee! Hamjambo kabisa hapo Halmashauri ya Wilaya/Mji?
 
Nimeona huo ubwabwa hapo jukwaani nikakumbuka enzi zetu za "gombania goli", unakuwaga mtamu asikuambie mtu! Hadi nimepata njaa sasa, ngoja nikapige lunch.
 
Hukumu ni tarehe 26.5.2012 tunasubiri tuone magamba watachakachua au la maana ushahidi unaotolewa hawawezi kuchomoka.
 
Huo ubwabwa umenikubusha vibudu walivyolishwa watu wa mwanza kwenye ile siku ya kuzaliwa magamba.
 

haiwezekani mlokole kuwepo CCM.
 
Ushahidi mwingine cku ya uchaguzi gari la mb rage tabora.lilipita baadhi ya vijiji na kutangaza kuwa mgombea wa cdm amejitoa kwenye uchaguzi.
 
Kesi hii isimamiwe vizuri ili liwe fundisho kwa wale wanaotumia ofisi zao na madaraka waliyopewa na umma vibaya.
 
kamanda Safari anasimamia Kesi...
Magamba lazima waende na maji...

========
Kesi imekaa vizuri kwa cdm lakini Prof Safari siyo courtroom lawyer. hajawahi kushinda kesi yoyote mahakamani. CDM wangemuunganisha na timi ya wanasheria ndipo atafanya kazi vizuri. ni mzuri kwenye timu kuliko kufanya peke yake. ni mwalimu mzuri wa sheria lakini si practioner wa mahakamani.
 
Hukumu ni tarehe 26.5.2012 tunasubiri tuone magamba watachakachua au la maana ushahidi unaotolewa hawawezi kuchomoka.
Una uhakika na trh hiyo mbona ni Jumamosi?
 
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, jana ilipokea ushahidi wa magazeti mawili, Mtanzania na Nipashe, ikiwa ni mwendelezo wa kusikiliza maelezo ya mashahidi kwenye kesi ya kupinga matokeo yaliyompatia ushindi Mbunge wa Igunga, (CCM), Dk. Dalaly Kafumu.

Shauri hilo lilifunguliwa na mlalamikaji Joseph Kashindye dhidi ya Dk. Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa serikalina msimamizi wa uchaguzi.

Mwandishi wa Mtanzania, Arodia Peter, alitoa ushahidi kuhusu habari ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Willson Mukama, aliyedai kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimepeleka makomandoo 33 Igunga ili wavuruge uchaguzi.

Arodia alitakiwa na mwanasheria wa upande wa mlalamikaji, Profesa Abdallah Safari, aieleze Mahakama ukweli kuhusu habari hiyo ambapo alidai kuwa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisi za CCM Wilaya ya Igunga, Mukama alisema Chadema wamepeleka makomandoo hao waliopata mafunzo ya kigaidi katika nchi za Afghanistan , Pakstan na Libya.

Ushahidi mwingine wa gazeti la Mtanzania, ulihusu ahadi zilizotolewa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kwamba atatenga bajeti maalum ya kujenga daraja la mto Mbutu pamoja na barabara nyingine iwapo wananchi wangempigia kura, Dk. Kafumu wa CCM.

Mwandishi wa Nipashe, Sharon Sauwa, naye alidai kuwa Waziri Magufuli alitoa ahadi ya ujenzi wa daraja la Mbuntu endapo wananchi wa jimbo hilo watachagua mgombea wa CCM.

Awali, wakili wa serikali na wakili wa mjibu madai waliweka pingamizi kuwa nakala za magzeti hayo visipokelewe kama vielelezo mahakamani.

Hata hivyo, Jaji anayesikiliza kesi hiyo, Mery Shangali, alitupilia mbali pingamizi hilo, akisema vielelezi hivyo ni sahihi kwa kuwa waandishi walioandika habari hizo wapo mahakamani kuvitolea ushahidi.

Jaji Shangali pia aliwataka mawakili wa upande wa wajibu maombi, wazingatie muda na kuacha maswali ambayo hayahusiani na mada inayozungumuziwa mezani ili kuokoa muda wa shauri hilo hivyo ushahidi huo kupokelewa.

Kesi hiyo itaendelea leo kwa mashahidi wa mlalamikaji kuendelea kutoa ushahidi wao.


CHANZO: NIPASHE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…