buswelu moja
JF-Expert Member
- Aug 24, 2014
- 226
- 180
KESI ya kughushi na kujipatia ardhi kwa njia ya udanganyifu iliyofunguliwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya katika kipindi cha serikali ya awamu ya tatu na ya nne, Danny Makanga dhidi ya mume mwenzake Mathew Molell imeanza kuunguruma katika Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha.
Hakimu wa mahakama hiyo anayesikiliza kesi hiyo, Mwankuga Gantwa juzi alimzuia mwendesha mashtaka wa serikali ,Mary Lucas kumuuliza swali shahidi wa kwanza ambaye ndio malalamikaji, Danny Makanga kwa kuwa swali alilouliza ni jipya na halimo katika maelezo yake.
Hakimu huyo alimzuia mwendesha mashtaka huyo pale alipomuuliza swali Makanga katika kesi ya jinai inayomkabili mme mwenzake, Mathew Mollel kuhusu kufuatilia mukhtasari wa serikali ya mtaa wa Levolosi unaodaiwa kughushiwa na kudai kuwa swali hilo jipya na halimo kwenye utaratibu.
“Sijaona mahali ambapo shahidi amesema alienda ofisi ya Serikali ya Mtaa kufuatilia nyaraka hilo ni swali jipya labda kama una swali jingine”, alisema Hakimu huyo.
Hakimu huyo alimwambia mwanasheria wa serikali na mara baada ya kauli hiyo mwendesha mashtaka huyo aliiambia mahakama hiyo kwamba hana swali jingine ndipo shahidi mwingine ambaye ni Haruna Fundikira (74)alifika mbele ya mahakama hiyo kutoa ushahidi wake.
Fundikira ambaye pia ni shahidi wa pili katika kesi hiyo ambaye ni Mwenyekiti huyo mstaafu wa serikali ya mtaa wa Levolosi alisema hajawahi kutoa muhtasari wowote ulioruhusu upatikanaji wa hati ya shamba hilo lililopo mita 200 Mianzini namba 231 block DD.
Fundikira, alisema pia hamjui Mollel na wala hajawahi kumwona na wala hajui kikao kilichoketi ofisini kwake juni 10 mwaka 2006 na kuruhusu mchakato wa upatikanaji wa hati ya shamba hilo.
Hata hivyo, alipoulizwa na wakili wa mshtakiwa, Ephraim Koisenge endapo anayatambua majina ya Joachim Kivuyo na Sara Kara ambayo yameandikwa ndani ya mukhtasari unaodaiwa kughuhiswa Fundikira alikiri kuyatambua majina hayo huku akisema kwamba Kara alikuwa ni katibu wake na kwa sasa ni marehemu.
Akiulizwa na wakili wa Mollel, Ephrehem Koisenge kuwa Mollel aliingiaje katika shamba hilo,Makanga ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi hiyo alikiri kumruhusu na kuendeleza shamba hilo na kujenga kibanda cha muda na baadae kuhamia na pia alikiri kumruhusu kumtafutia hati katika Halmashauri ya Manispaa ya Arusha {sasa Jiji}.
Wakili alimuuliza shahidi huyo kuwa Mollel ameshitakiwa na kosa gani katika mahakama hiyo ,shahidi huyo alisema kuwa ameshitakiwa kwa kosa la kughushi muhutasari wa serikali ya mtaa wa Levolosi na kujipatia hati na alipoulizwa anadai nini mahakamani hapo alisema kwamba anadai eneo lake la kiwanja.
Hata hivyo, shahidi wa tatu katika kesi hiyo, Amina Hassan aliiambia mahakama hiyo kwamba anamtambua Mollel kama mume mwenza wa Makanga na mara kwa mara Makanga amekuwa akiwasili jijini Arusha na kufikia kwa Mollel.
Shahidi huyo aliiambia mahakama kwamba anakumbuka mama yake mzazi(Halima Hassan) ambaye ni marehemu aliwahi kushuhudia akimpatia nyaraka mbalimbali Mollel kwa lengo la kushughulikia hati ya kiwanja hicho wakati alipoleta mbao katika eneo la kiwanja hicho wakati akiwa katika hatua za ujenzi katika kiwanja hicho.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali alitoa taarifa ya kuwasilisha kivuli cha baadhi ya nyaraka kutumika kama ushahidi katika kesi hiyo na kesi hiyo itasikilizwa tena machi 27 mwaka huu ambapo shahidi mwingine ambaye ni ofisa wa jeshi la polisi mkoani Arusha ,Sajenti George atapanda mahakamani kutoa ushahidi wake upande wa jamhuri.
Mwisho