Kesi ya DC Makanga yakwama, Wakili augua mafua ghafla

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
752
1,810
Kesi ya kughushi mukhtasari wa serikali ya mtaa wa Levolosi jijini Arusha iliyofunguliwa na mkuu wa wilaya, Dahni Makanga dhidi ya mfanyabiashara, Mathew Mollel imeshindwa kuendelea mahakamani baada ya mwendesha mashtaka wa serikali, Mary Lucas kuugua ghafla mafua.

Kesi hiyo nambari 430 ya mwaka 2016 ilikuwa imekuja mahakamani hapo kwa ajili ya mashahidi wawili kati ya sita upande wa serikali, Joachim Kivuyo ambaye ni Katibu wa Baraza la Ardhi la kata ya Levolosi na Mohammed Hassan kutoa ushahidi wao.

Hatahivyo, wakili wa serikali, Grace Medukenya alimweleza hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Gantwa Mwankuga wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha kwamba mwendesha mashtaka wa serikali, Lucas kwamba ni mgonjwa na hatofika mahakamani.

Wakili Medukenya aliiomba mahakama hiyo ihairishe shauri hilo kwa kuwa mwendesha mashtaka katika kesi hiyo ameugua ghafla ugonjwa wa mafua kusema hatofika mahakamani hapo.

Mara baada ya ombi hilo hakimu Gantwa alisema kwamba mahakama imekubaliana na ombi hilo na kuiharisha kesi hiyo hadi Mei 2 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kusikilizwa na kuwataka mashahidi kuhakikisha wanafika mahakamani hapo bila kukosa.
616d9b579fe4b09bf5ef77e804d1ba29.jpg
 
Back
Top Bottom