Kesi, Mahakama na mahabusu ndiyo maendeleo kwa CHADEMA?

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
37,551
47,205
Bila shaka wabunge wa chadema walipokua wakipiga kampeni kuomba kura majimboni kwao! Walitoa ahadi tamu sana na kuwapa imani wananchi waliowachagua kuwa watawaletea maendeleo ambayo ccm walishindwa kuwaletea, wananchi nao wakadanganyika na kuwachagua!

Sasa hali imekua tofauti kabisa, zile ahadi tamu hazitekelezeki, kilichopo ni mfululuzo wa kesi za kujitakia , kushinda mahakamani bila sababu za msingi na kukaa mahabusu kuliko na faida!

Inasikitisha sana kwakua lengo la wananchi halijatimia mpaka sasa, sidhani kama kuna mwananchi anayetaka mtu akakae mahabusu kwa mbadala wa maendeleo aliyoyaota kupitia kura yake, bila shaka hakuna hata mmoja anayetaka umaarufu wa kushinda mahakamani kwa mbadala wa kituo cha afya ambacho mbunge huyo alimuahidi wakati akimuomba kura!

Nina imani kabisa kuwa wananchi hawafurahishwi na tabia hii , na watachukua maamuzi kwa kuwaondoa wabunge mzigo! Kwa kuwaondoa wabunge wanaotafuta umaarufu binafsi wa magazeti na TV na kuwasahau waliowatuma!

Kesi, mahakama na mahabusu ndio maendeleo waliyokuwa wakihubiri chadema?
 
Mlikuwa mnataka kutumia mahakama ili kutumiza mihemko ya kiongozi wenu. Bahati mbaya kuna baadhi ya majaji hawaburuzwi, sasa hivi ndio unakuja na hizi swaga za kishamba. Kuna majimbo kibao ni masikini sana na yanaongozwa na wanaccm ambao hawahawahi hata kukanyaga mahakamani, unatuambiaje kuhusu hali hiyo ya umasikini. Kajifunze propaganda upya, mlitaraji kumweka ndani Lema watu watampotezea lakini watu hawadanganyiki. Halafu kwa taarifa yako maendeleo yanaletwa na serekali na sio mbunge.
 
Waulize wanaowafungulia viongozi wa CHADEMA kesi kila kukicha hala wanaangukia pua
 
Back
Top Bottom