KERO ZA WAENDESHA BODABODA

Siempre Hechos

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2016
Posts
1,231
Reaction score
1,538
Uendeshaji bodaboda i umerahisisha usafiri kwa kiasi falni na pia umeajiri vijana wengi na baadhi yao umewapunguzia ukali wa maisha na pia kuachana na vitendo vya uvunjifu wa sheria kama wizi (japo wapo wanaotumia fursa hii kuwa wezi wazuri). Lakini katika ajira yao hii kumekuwa na kero kadha wa kadha hasa wanapokuwa njia kuu kama ifuatvyo japo kwa uchache;

1. Wanaongoza kuvunja sheria za barabarani (kwenye makutano ya barabara na hasa kwenye taa za barabarani wengi hawazieshimu) na kusababisha ajali za makusudi. (Afisa usalama barabarani wanawaangalia tu)

2. Wanaharibu magari ya watu eidha kwa kukwangua rangi au kuvunja kabisa baadhi ya vifaa kama side mirrors na taa hasa pale wanapopita katikati ya magari kwa tahadhari dhaifu wakiwa mwendo mkali.

3. Wanaover-take karibu kabisa mbele ya gari inayotembea bila tahadhari ya kutosha kwamba lolote linaweza kutokea kwamba anaweza kuteleza akasababisha kugongwa na gari.

Serikali tunaomba wawangalie sana hawa watu, wamejipa uhuru na mamlaka makubwa sana ya kufanya watakavyo hata pale wanapokuwa wamekosea wao, ajali inapotokea kati ya gari na boda boda hualikana kwa wingi na kufanya uharibufu kwa upande wa pili kisa tu mwenzao kapata ajali kati yake na mwenye gari. Hili ni bomu, isipochukuliwa kwa umakini mkubwa, vitendo vyao vya uharibifu wanavyofanya vitageuka kuwa uhalifu uliohalalishwa.

Karibuni kwa mjadala.
 
Mkuu...
Wewe ni abiria wa bodaboda, dereva wa bodaboda ama unamiliki hizo zenye wanazo ovateki kwa karibu na ama kukwangua rangi...!!??
Ili nichangie huu mjadala, ningependa kwanza kujua wewe upo kundi lipi kati ya hayo makundi ya above
 
Mi ni abiria wa boda boda japo sio mara nyingi mkuu!
 
Mi ni abiria wa boda boda japo sio mara nyingi mkuu!
Sawa mkuu...
Basi naomba nikushauri tu uachane na kupanda bodaboda ili ujiepushe na virendo hivyo hatarishi.
 
Sawa mkuu...
Basi naomba nikushauri tu uachane na kupanda bodaboda ili ujiepushe na virendo hivyo hatarishi.

Nitajitahidi kupunguza mkuu matumizi ya huo usafiri mkuu sio kuacha kabisa si unajua usafiri wwakati mwingine unavyosumbua, sina jeuri ya kuacha kabisa kutumia usafiri wa boda boda.
 
Wanachonikera mimi hawa jamaa ata sehemu za watembea kwa miguu wao wanaona sehemu zao za kupitishia bodaboda! Sehemu wanazopack utakuta wamefunga barabara yote kisa wao wamepack hasa kwenye makaravati ndiyo wanapenda
 
Mkuu...
Wewe ni abiria wa bodaboda, dereva wa bodaboda ama unamiliki hizo zenye wanazo ovateki kwa karibu na ama kukwangua rangi...!!??
Ili nichangie huu mjadala, ningependa kwanza kujua wewe upo kundi lipi kati ya hayo makundi ya above

Wewe ovyoooo changia mada acha akili yako ya ubodaboda
 
Nusu saa haijaisha nimetoka kushuhudia bodaboda wamegongana wao kwa wao kwenye makutano ya barabara na walikua wao wawili tu wala hakuna gari wala nini. nimeacha wanagala gala chini.
 
Wewe ovyoooo changia mada acha akili yako ya ubodaboda
Mkuu, nimelazimika kupitia threads zako kabla ya kukujibu.....
Nilicho kigundua ni kwamba, hivi ndivyo ulivyo.
 
Pamoja na mambo uliyo ya ainisha yana ukweli, lkn ukweli wa nusu ya uliyoyaeleza yanachangiwa na jamii mzima. Kwa mfano ukiwa unaendesha bodaboda na ukafuata foleni kama gari zilivyo basi mwenye gari wa nyuma atakushangaa na atakughasi kwa honi nyiingi huku akilalama, ukimuuliza nini shida atakujibu we huoni mpenyo huo tembea. Hii maaana yake hata wenye magari wamekosa mpenyo tu kutokana na upana wa gari lake vyenginevyo hata wao wasingekaa ktk line. Hill ni moja tu yapo mengine mengi huchangiwa na jamii mzima.
 
Pole mkuu, pia wana overtake hovyo hovyo tu, iwe kulia au kushoto wao haijalishi, wanapiga honi kijinga kijinga, wanafungulia radio zao kwa sauti kubwa, wale wa kuvaa ndala, kutokuwa na helmet bado wapo, bado wengi wao ni wezi, pia bado wengi wao ni wachafu na kunuka, wengi tena wanaendesha wakiwa wamelewa, mwendo wao una kasi ya ajabu..ni janga la taifa kwa kweli...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…