Mkuu ukienda Iringa hapo mikumi utachoka,kama una manual car bas tab tup,kama ukienda Dodoma ndo usiseme hapo kongwa yameongozana kama milima ya udzungwa!Mkuu umenena kunasiku nilitaka kuanzisha thread hapa kuwa barabara yenye humps nyingi kuliko zote ni ile ya kutoka Himo - Moshi Mjini, ikifuatiwa na ya kutoka Segera - Tanga kwa mtazamo wangu. Kama unatakwimu nyingine tafadhali tuwekee ili tujue nasi.
Yaani humps hizi ni kitisho kwanza ni kubwa kuliko maelezo na mengine ni kama ulivyosema zinapoteza muda, kuharibu magari n.k
Mkuu sijui na hao Tanroad manager wanazipasisha kwa kigezo gani?Niliwahi kumsikia Magufuli akiagiza ziondolewe hususan za kwenye service road lakini mpaka leo sijaona juhudi zozote zinazofanyika kuhusu hivi vikwazo vya barabara. nafikiri maagizo haya yanakuwa yamekaa kisiasa sana kuliko uhalisia wake! nafikiri uwajibikaji ni tatizo ya msingi hapa Bongo! sijui tatafika lini? mungu bariki TZ