Nimekata tiketi ya bus ( Classic coach) siku tatu kabla ya safari kutoka Moro kwenda Mbeya. Tiketi inasema safari ni saa 12 asubuhi ila muda wa kuwasiri ni saa 11:30 asubuhi. Nimewasiri saa 11: 30 stendi nimeambiwa nisubiri gari. Cha ajabu nimesubiri mpaka saa 1: 10 asubuhi nakuja kuambiwa et gari ilipita saa 11: 20 kwa hiyo nitapakiwa kwenye gari jingine.
Hivi hakuna njia au sehemu ya kuripoti haya matatizo ya abiria ikiwezekana hawa watu wawe wanachukuliwa hatua za kisheria.