DOKEZO Kero ya taka ni kubwa Unguja. Wanaokusanya hawatimizi majukumu yao

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Wakaazi wa Unguja, Zanzibar tuna kero kuhusu hawa wahusika wa ukusanyaji taka, wanaziweka karibu na makazi ya watu, taka zinanuka sana na zinakaa zaidi ya mwezi pasipo kuzolewa na wahusika.

Tunapata shida sana, sehemu ya kuishi ndio wanaweka dampo hii si sawa hata kidogo, tunaumia.

Masheha wa maeneo hayo wala hawana habari na hilo japo taarifa tunawapa lakini wanatupotezea.

Serikali iangalie namna ya kufanya kuhusu hii changamoto.

Mtaani kuna stori kuwa kuna kampuni amayo ilipewa tenda na imemaliza muda wake, hivyo kwa sasa hakuna usimamizi kwa kuwa mchakato umerejeshwa Serikali za Mtaa ambazo nazo hazitilii maanani kinachoendelea.
 
Serikali ya hovyo na viongozi wa hovyo, sisi tuna miezi 2 gari la taka halijapita jiulize taka tunatupa wap. By the way tuendelee kuiamini chama CCM mbele kwa mbele. Period
 
Wakaazi wa Unguja, Zanzibar tuna kero kuhusu hawa wahusika wa ukusanyaji taka, wanaziweka karibu na makazi ya watu, taka zinanuka sana na zinakaa zaidi ya mwezi pasipo kuzolewa na wahusika.

Tunapata shida sana, sehemu ya kuishi ndio wanaweka dampo hii si sawa hata kidogo, tunaumia.

Masheha wa maeneo hayo wala hawana habari na hilo japo taarifa tunawapa lakini wanatupotezea.

Serikali iangalie namna ya kufanya kuhusu hii changamoto.

Mtaani kuna stori kuwa kuna kampuni amayo ilipewa tenda na imemaliza muda wake, hivyo kwa sasa hakuna usimamizi kwa kuwa mchakato umerejeshwa Serikali za Mtaa ambazo nazo hazitilii maanani kinachoendelea.
Ni kweli hii inakera sana utakuta taka wanakusanya na kuweka ovyo mitaani alafu kwenye kudai hela kwa haraka na mapema ukichelewa kulipa unatoleshwa faini ila kuhusu taka zinazozagaa hamna faini kiufup tunaumizwa na hili taasisi husika zijitahidi t katika hili kuweka jiji letu safi na pia kuepuka kusambaa kwa maradhi ya mlipuko ikiwemo kipindupindu
 
Back
Top Bottom