KERO: Usumbufu wa makonda na wapiga debe wa daladala kituo cha kilombero jijini Arusha

Twalyaninkomi

JF-Expert Member
Oct 31, 2016
265
259
Kheri Jf!

Nimepata kufika jijini Arusha kikazi kwa muda wa siku 5 tu, leo siku ya tatu yaaani kero kubwa kwa watumiaji wa usafiri wa umma (daladala) jijini hapa ni katika kituo kidogo cha daladala kilombero kilichopo katikati ya jiji.

Kiukweli wale vijana wapiga debe ni kero kubwa, yaani mtu asikatishe yale maeneo ni lazima wamsumbue kwa kelele za twende huku twende huk na hapo ukiwa legelege ndio kabisa utaishiwa kuvutwa na kupakizwa kwenye gari hata kama si msafiri!

Kwa hali ya kawaida wale vijana hawana ulazima wa kuwepo pale kwani usumbufu kwa abiria na wapita njia, pia gari zote zimeandikwa wapi zinaelekea hivyo abiria wengi wanaelewa wapi na gari gani wanatakiwa kupanga!

Rai yangu kwa wahusika, ondoeni kero hii wale vijana wafanye kazi zingine za ujenzi wa taifa.
Hii hali imebaki Arusha tu ni usumbufu kwa kweli

au na hili linasubiri tamko toka lwa mkulu?
 
Huku Dar sie abiria wa mbagala ndio tunakimbilia na kugombania mabasi!
Hii ndio kero yetu kubwa, hao vijana lazima ni vibaka wa chadema tu maana Arusha yamejazana kweli
 
Hiyo ndio chadema bwana.

Wako bize kurusha matusi na kutoka nje ya bunge badala ya kushughulikia matatizo ya wananchi waliowachagua.
mkuucnafikiri hili swala sio la kuiachia chadema kwa sababu ya jimbo hili liko chini yake!

serkali kwa ujumla wake walishughulikie hili kwa pamoja jiji litakua safi
 
Back
Top Bottom