KERO KERO Sugu ya Maji Mwanza (Nyegezi)

KERO KERO Sugu ya Maji Mwanza (Nyegezi)

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunapenda kuwakumbusha kuwa ni takribani mwezi mmoja sasa tangu Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alipozindua rasmi chanzo kikuu cha maji kwa Jiji la Mwanza — tukio ambalo liliibua matumaini makubwa kwa wakazi wa maeneo mengi yaliyokuwa yakisumbuliwa na kero ya muda mrefu ya maji safi na salama.

Ni ukweli usiopingika kuwa siku ya uzinduzi, maji yalifika maeneo mbalimbali ikiwemo Nyegezi na maeneo ya jirani yaliyokuwa na historia ya ukame wa maji. Tulifurahia sana tukiamini tumefunguliwa ukurasa mpya wa ustawi wa kijamii na kiafya.

Hata hivyo, baada ya ziara ya Mheshimiwa Rais kumalizika, hali imebadilika kabisa. Maji yamepotea tena, na kero imekuwa mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa awali. Kwa zaidi ya mwezi sasa, wakazi wa Nyegezi hawapati maji hata kwa mgao. Tunajiuliza maswali mengi:

Kuna tatizo gani la kiufundi au kiutendaji?
Ni kwamba miundombinu haijakamilika au kuna ucheleweshaji wa makusudi?

Kwanini maji yanapatikana kwa saa 24 maeneo ya Shinyanga lakini Mwanza – chanzo chenyewe – hali ni mbaya zaidi?

Je, huu ni uzembe, au kuna hujuma dhidi ya juhudi za Rais wetu mpendwa?

Tunaiomba Wizara ya Maji, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) pamoja na Viongozi wa Mkoa na Jiji la Mwanza wachukue hatua za haraka:

1. Kufanya uchunguzi wa kina kuhusu hali halisi ya usambazaji maji katika Jiji la Mwanza na kutoa taarifa kwa umma.

2. Kuwajibisha wahusika endapo kuna uzembe au hujuma. Kufikisha maji kwa mgao wa haki angalau wakati huu ambapo mfumo mpya unafanyiwa maboresho.

3. Kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi huu muhimu kwa wananchi.

4. Tunasema haya kwa nia njema, tukiamini kuwa Serikali yetu sikivu haitaruhusu mafanikio ya miradi mikubwa yaharibiwe na watu wachache au mifumo duni isiyojali wananchi wa kawaida.

KERO YA MAJI NI KERO YA UHAI. Tunahitaji suluhisho sasa.
 
Kero ya maji jiji la mwanza na viunga vyake tumeimalizaa tayari Uo ni uchochezi wakuigombanisha serekali na wanaichi tutakukamata utajutaa mi 5 tenaaaaaaaaaa in Majaliwa voice
 
Mwanz maji ni kama dhahabu Jamii forum hii mada imekua ikijirudia sana huku wanini msiunde timu yenu iingie mjini hapo ichanganue ione ukweli wanachi wanvyo sota?
 
Nimeona mwingine tena wa mkolani analalamikia hili. Nadhani muungane na viongozi wa serikali za mitaa muende kumuona mkurugenzi wa MWAUWASA. Hiyo hali haikubaliki.
 
Ndiyo maajabu yenyewe hayo!!

Hii nchi maji ya bomba kuendelea kuwa ya kusuasua ni aibu hata kwa mikoa ya Singida na Dodoma.
 
Back
Top Bottom