Kero: Sitaki kuitwa mwalimu, kama hunijui jina kaa kimya

shonkoso

JF-Expert Member
Mar 13, 2015
687
1,455
Habari za kuitana oah teacher teacher au mwalimu, wakati watu tupo na mishe zetu siyo sawa kabisa, mimi nilishasema, ruksa kuniita teacher sijui MWALIMU KAZINI TU.

Mtu upo na mizinguko yako town unasikia limtu tichaaaa, wewe hunijui jina kama unaona jina langu gumu basi niite hata wewe.

Au Mara nyingine mpo kwenye kamati za harusi na lijitu kwa makusudi utasikia mwl, wewe mimi siyo mwl wako nikome, yaani unanitangaza kila mtu ajue mimi ni cheap labour wa serikali.

Tutunziane heshima tafadhali.
 
kweli jamaa ni mkuda, angekuwa mwalimu asingeadika hapa, kwa sababu wanaomwita hawapo humu
 
Hahaaaa, enzi za mwalimu kila mtu alipenda kuitwa Teacher, tena ukiitwa mwalimu unatembea kwa kutanua mikono na kifua mbele kabisa,, nafikiri ni kipindi uzalendo ulipokuwa juu sana,, kila kada serikalini ilikuwa na uchumi karibia sawa.

Katika zimwi la ubepari tulilo nalo sasa hv kila mtu anatamani kuwa katika sekta ambayo atazipiga kwa haraka na kuwa milionea.

Ukweli ni kwamba kama unapenda kazi yako utafurahia kuitwa Teacher hata kama utakuwa na mrembo wako karibu yako. Tuache kujikataa na kufeel inforior kwenye kada tunazofanyia kazi,, unaweza fanikiwa popote ulipo. Jikubali, jipange, fanikisha mipango yako ya maendeleo.
 
Walimu hawako hivyo , wewe sio Mwl ila umeamua kutumia jina la Mwl ili upunguze machungu yako, kwa taarifa yako hakuna watu wanajisikia faraja kuitwa kwa majina ya vyeo vyao kama walimu
 
tichaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa wazee wa back bench tunakulia buyu utoke class tukupe namba ya dgo first year............................
 
Habari za kuitana oah teacher teacher au mwalimu,wakati watu tupo na Moshe zetu siyo sawa kabisa,Mimi nilishasema,ruksa kuniita teacher cjui MWALIMU KAZINI TU, MTU upo na mzinguko yako town unasikia limtu tichaaaa,wewe hunijui jina kama unaona jina langu gumu basi niite hats wewe,au Mara nyingine mpo kwenye kamati za harusi na lijitu kwa makusudi utasikia mwl,wewe Mimi siyo mwl wako nikome,yaani unanitangaza kila MTU ajue Mimi ni cheap labourer wa serikali,tutunziane heshima tafadhari
bas sawa....
 
Bora wakuite mbunge au diwani maana wataanza na kibwagizo cha mheshimiwa sio mtu anakurupuka tu anakuita Afande ..!
 
Ok, ntakuita mkuu, sio mwalimu, japokuwa ,kuitwa mwalimu kipindi hiki ni kama kupigilia msumali kwenye kidonda hasa sie wa HKl,japokuwa tunaweza kujifariji kuwa president pia in teacher kuna kahaueni ka kimadaraka

*Ok mkuu unankumbusha kipindi nipo skul, maticha wa field wakija kutupigisa pindi badaye wanatwambie tukikutana kitaa tusiitane teacher has a sijui walitaka tuwaitaje sijapata jibu hembu twambie tukuitajeee,*
 
walimu wengi hawakupenda na wala hakutarajia kuwa walimu ila basi tu kwa sababu ya umasikini ili apate uhakika wa ajira au kiwango cha chini cha matokeo ndicho kilichompeleka
dah!! pole sana ndio maisha uliyoyachagua au yaliyokuchagua
 
Mwalimu shonkoso tutunziane heshima 'tafadhali' tuanzie hapo kwanza! Lugha hii wajameni!
 
Back
Top Bottom