DOKEZO Kero katika huduma ya afya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Primers one

Member
Joined
Sep 23, 2024
Posts
14
Reaction score
10
Hospitali ya (w) Mpwapwa ni moja ya hospitali ya umma yenye duka lake la dawa. Cha kushangaza zaidi unakuta kwenye dirisha la dawa la hospitali hakuna dawa ila kwenye duka la dawa la hospitalini kuna dawa. Na zaidi mgonjwa anaelekezwa akanunue dawa kwenye hilohilo duka la hospitalini.

Pili, wajawazito haswa wa upasuaji, mtu unaandikiwa dawa na vifaa halafu haviji kutumika, vinafichwa. Mtu kila ukienda kusafisha kidonda unaandikiwa vifaa vingi na pia lazima ulipie kusafisha kidonda kila ukienda. JE, NI SAHIHI?

Mpwapwa tunaumia na huduma ya aina hii. Serikali na wadau tusaidieni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…