Kero barabara ya Morogoro

Kero barabara ya Morogoro

kyoga

Member
Joined
Sep 16, 2011
Posts
31
Reaction score
11
Barabara ya Morogoro toka Kimara kuja mjini imekuwa ni kero kwa watumiaji, kwa muda mrefu sasa. Ujenzi unaoendelea kwenye barabara hiyo umesababisha usumbufu mkubwa sana kiasi cha kuwafanya watu watumie masaa matatu hadi manne kufika posta au kariakoo.

Naomba viongozi wanao husika waliangalie hili, ebu wa waangalie hawa jamaa wanaojenga hii barabara, mfano pale kimara wamebana baraba ya mchepuko na kusababisha magari kupita kwa shida bila sababu za msingi wala hawana mpango wa kutengeneza vizuri Diversion ili kuhakikisha magari yanapila kwa urahisi.
 
Viongozi gani? Wao wanakaa Oysterbay na Masaki habari za Kimara yaani ni kama unawaambia habari za nchi nyingine.Kinachotuponza sisi Watanzania ni uoga wa kuthubutu, hivi siku moja tukiamka asubuhi tukafunga barabara yote kwa maandamano kwamba mpaka kieleweke unafikiri hakuna hataua inayoweza kuchukuliwa. Mfano pale Ubungo mataa panaweza kufunguliwa pakawa panaruhusu magari yote
 
Hapa kuna sabotage ambayo wahusika yaani viongozi hawana uwezo wa kuiona. haiwezekani barabara yenye hadhi kama hii ijengwe kwa masaa nane tu kwa siku na weekend hakuna kinachoendelea
 
Nimepita sahivi pale maeneo ya kibo kuna lori limepanda vile vizingiti ikatokea upande wa pili.

Kale kabarabara kadogo sana hadi kero ukipishana na gari lenye speed kali au lori la masafa utajuta
 
ndo viongozi wenu walivunja barabara nzuri na kutia kwenye shida. Akili ndogo kuongoza kubwa yaani hii barabara ingeachwa kama ilivyokuwa hizo gharama zikatumika kutengeneza barabara mpya ningeona wana akili.
 
Back
Top Bottom