Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Nimemskia rais wa Kenya katika kipindi cha television ya NTV ya kenya ajijinasibu hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi yake kwa maneno yenye ukweli na uchungu unao uma na nimeelewa kwanini hatuajiri tukisingizia uhakiki.
Kasema yeye kwa nchi yake 100% ya kodi inalipa matumizi yote ikiwepo mishahara ya watumishi wa umma na inabaki kwa ajili ya uwekezaji na hawategemei wagadhiri kuendesha nchi ila walipa kodi wanatosha.
Na akasema ukingalia nchi kama Tanzania, Uganda wao zaidi ya 40% wanategemea wahisani ndo wajiendeshe hasa kulipa mishahara na kuhudumia jamii.
Na kasema wametofautisha utendaji yaani professionals wanafanya kazi yao hawaingiliwi na wanafanya vizuri na siasa inabaki kuwa siasa, na siasa haingilii professional ya mtu.
Nikawaza:
Huu uhakiki ulikuwa feki baada ya wahisani kukata misaada juu ya uchaguzi wa 2015 wa kung'ang'ania madaraka na hapa kwetu watendaji sifa uwe kada wa chama na alisema ni lazima uwe upande wake ndo uongie katika utwndaji. Wao wana ukabila, ufisadi lakini ikija kwenye swala la utaofa wako mbele huku chama kwanza then taifa baade.
Ni ukweli mchungu