Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,936
KENYA WANATENGENEZA KISINGIZIO KWA MACHAFUKO MENGINE YA UCHAGUZI WAO WA MWAKANI
TUHUMA za Mbunge wa zamani wa Jimbo la Starehe jijini Nairobi Kenya, Maina Kamanda kuwa Rais John Pombe Magufuli na Rais Salva Kiir wa Sudan ya Kusini wanamfadhiri Raila Odinga kuhochea vurugu Kenya ni upuuzi na kichekesho cha karne.
Ni ushauri wa bure kwa ndugu zetu wa Kenya wawe wanachagua viongozi wenye historia. Maina ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP) cha Kenya, alipata kuwa meneja msaidizi wa hoteli jijini Nairobi.
Wakati wanachinjana tangu uchaguzi wao wa 2007 na ule wa March 2013 hadi watu zaidi ya 1,200 wanauawa, Magufuli na Kiir walihusika? Huyu Maina simwelewi kabisa.
Kenya huwa wanachinjana katika kila uchaguzi. Sasa hivi, wanajaribu kutengeneza kisingizio cha machafuko ya uchaguzi wao wa mwakani. Bahati mbaya ni kisingizio cha kitoto.
Huko ICC Kenyatta na Ruto walipelekwa kwa sababu gani? Wakati JK alipokwenda kuwapatanisha baada ya Uchaguzi wao mkuu wa 2007, wakaanza kutwangana, Magufuli alikuwa Rais wa Tanzania?
Waache visingizio vya kitoto. Huo ni usanii mtupu. Watatue matatizo yao wenyewe wasianze ujinga wa kutuingiza kwenye kushindwa kwao. Labda wangekuwa wastaarabu waombe tuwapatanishe.
Mandela aliwahi kusema, "Maadui wako sio lazima wawe maadui wangu." Hii ni mbinu ya kitoto ya kujaribu kufanya Raila Odinga abaguliwe na watu wanaomheshimu. Ni mbinu mbovu isiyozingatia taratibu za kidiplomasia na inayotishia mustakbali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Lakini pia inaweza kuwa hasira zakukosa tenda ya ujenzi wa bomba la mafuta na ujenzi wa reli ya Rwanda kuunganisha na njia ya Tanzania.
MwanaJF.