Kiwango cha thanani ya pesa hakina uhusiano na utajiri au umaskini wa nchi. Kwa mfano Japanese Yen ni shilingi 18.24 za Tanzania au shilingi 0.913 za Kenya, lakini Japan ni moja ya mataifa tajiri kabisa duniani. Ni kama ya tatu au ya nne kwa utajiri duniani. Kwa kifupi unaweza kuipa thamani kubwa pesa yako lakini usipate mtu anayeihitaji hiyo pesa yako kwa biashara zake kama huna kitu cha kumfanya mtu aihitaji hiyo hela yako!