Kenya huwa tunajivunia our diversity na huo uwezo wa kuwa na jamii zinazoongea lugha nyingi na desturi nyingi tofauti. Na hizi jamii zimekua zikitaniana tangu jadi, ni pale tu wanasiasa walikoroga na kuweka uhasama baina yetu, ila wengi tunapenda tamaduni zetu.
Mimi kama Mkikuyu nilipenda sana enzi zile AFC na Gor walikua wakicheza miaka ya themanini, ilikua raha sana maana utani ndio ulikua unanoga kweli. Binafsi nilikua shabiki wa Rivatex, lakini michuano ya AFC na Gor ilileta raha nchi yote. Tulipenda sana huo utani wao. Tatizo wanasiasa waliingilia na kuharibu mengi. Pia ikumbukwe, kuna jamii huwa zimebarikiwa vipaji fulani, kama jinsi unapata wanariadha wengi wametokea kwa jamii ya Wakalenjin.
Hata Tanzania pia ni vigumu kumpata Mchagga anacheza soka. Wao wamebarikiwa kwenye ujasiriamali na wachakarikaji, Wakurya na Wameru wapo sana kwenye jeshi maana wagomvi na wazushi sana. Waswahili (makabila ya Pwani) wacheza viduku usiku, makabila ya Kigoma wasanii wa nyimbo, Wasukuma washirikina fika n.k. orodha ni ndefu.
Utakuta mtu wa jamii fulani hata akizaliwa ndani na katikati ya jamii tofauti na ya kwake, ila ana tabia fulani ambazo si za hapo alipo.