MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
These are the six most powerful people in Tanzania!
Kwa nchi kama Tanzania ambayo ina taasisi zisizo imara, Hawa ndiyo macho, masikio na maisha ya Rais magufuli.
Ni kweli madaraka ni dhamana lakini kwa nchi kama Tanzania, madaraka ya juu ni zaidi ya dhamana.
Kelele anazopiga Rais Magufuli kuhusu kubomoa watu ambao watamkwamisha katika kazi zake yatakuwa hayana maana yoyote kama yatakuwa hayajapata baraka kutoka kwa hawa Watanzania ambao wako sita.
Hiki ni kikundi cha watu wanaoifahamu vizuri Tanzania na kuna wengine kati yao hata ukichukua picha yake na kuanza kuwahoji Watanzania kama wanawafahamu, ninaamini ni watanzania wachache wanawafahamu.
Mmojawapo kati yao anaweza kuibadilisha Tanzania kutoka utawala wa kiraia mpaka utawala wa kijeshi. MwL. Nyerere anafahamu vizuri kutokana tukio lililotokea Tarehe 20 Januari 1964.
Mmojawapo kati yao anaweza kufanya maisha ya raia au kisiasa kwa wanasiasa kuwa niya wasiwasi nchini. Viulize vyama vya siasa kwa kinachotokea kwa sasa.
Mmojawapo ana uwezo wa kufahamu hali halisi ya kiusalama nchini na pia ana uwezo wa kumzuia au kumruhusu Rais Magufuli kwenda sehemu yoyote na wakati wowote iwe nchini au nje ya nchi. Muulize Mzee Peter Bwimbo, aliyekuwa mkuu wa kitengo cha ulinzi wa viongozi, (Presidential Securty Unit) wakati wa utawala wa Mwl. Nyerere.
Mmojawapo anaweza kufanya maisha yako gerezani kuwa mazuri au mabaya. Muulize aliyekuwa Waziri wa fedha Basil Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona.
Mmojawapo kati yao anaweza kuzifanya kazi zako au biashara zako kuwa katika wakati mgumu kama akiamua kukufuatilia kwa karibu. Muulize Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola, Mbunge wa Lupa Victor Mwambalaswa na Mbunge wa jimbo la Mvomero Sadick Murad.
Mmojawapo anaweza kukuruhusu kuwa Mtanzani au la. Muulize Jenerali Ulimwengu.
Kinadharia (theoretical) unaweza kutokubaliana na angalizo langu lakini kiuhalisia (practical) huwezi kupambana na ukweli wa angalizo langu.