Kelele za dar live mbagala

Mi nadhani watu hamjajua uzuri matumizi ya sheria...nenda mahakamani iombe mahakama imlazimishe kuzima mziki,,,sheria za mdhara au TORT LAW...zinaapply mimi nimewahi kupambana na mwengne pale mwenge nikamshinda na akafunga bar...
 
hiyo hata ukalalamike ikulu, utapoteza nguvu zako bureeeeeeeee
 
Dar Live ina mkono mrefu wa Riz 1. Haiwezi kufungwa hata watu wakifa kwa kelele labda M4C wachukue nchi.
TAFAKARI, CHUKUA HATUA

Kuna siku huyo Riz1 mtamaliza vya kumpa mtasema ana mkono hata kwa mama zenu.
 
Tena kaeni kimya msiongee kwani mtahaishwa kwa kuambiwa eneo hilo ni la wazi na zakeem itabaki kama recreational grounds we vumilia tu kukaa huko ipo siku utakaa masaki
 
Uwanja wa Taifa wa burudani ulitegemea uweje tena mkuu wangu? ila mimi nimefanikiwa kuifunga Night club jirani yetu ilikuwa ikikesha na kutusumbuwa na muziki usiku kucha, nikamwambia OCD wetu kama amechoka kukaa Dar es salaam basi aendelee kula rushwa za yule mwenye ukumbi halafu ndio atajuwa nini maana ya panguwa panguwa. sasa hivi kimya saa 5 kamili wanafunga adabu na heshima.
 
Kuna siku huyo Riz1 mtamaliza vya kumpa mtasema ana mkono hata kwa mama zenu.

:focus:

Acha kutetea mafisadi Riz1 ni fisadi ndani ya mwaka m1 hauwezi kuwa billionea haiwezekani kwa kazi gani? IMMA ADV?
 

Kazi nzuri kamanda! Nakumbuka wiki kama mbili zilizopita kulikua na uzi mwingine hapa,yakilalamikiwa makelele ya mikesha ya makanisa ya kilokole na hadhana za alfajiri. Nchi na Dunia kwa ujumla tunapita ktk mabadiliko makubwa ya kijamii,kitekinolojia na sayansi. Wapiga kelele kwasababu zozote zile wajiandae kupelekwa ktk vyombo vya sheria kama watataka kuendelea kuishi kama wenzetu karne kadhaa zilizopita.
 
Yeye analalamikia kelele za huo ukumbi sasa kama gesti za huko kwenu zina kelele toa dukuduku lako na wewe

Wale wanaolala (??!!) wakinogewa hawaipigi kelele??
 
Naomba kwa hili wana jamii tushirikiane maana watu wa mbagala wanakosa haki zao za kupumzika jamani tunaumia sana ukienda polisi hawakusikilizi sasa tuganyeje je tukitumia nguvu kuondoa kwa mikono yetu itakuwaje maana hata vijana wetu na mabinti wanajiuZA na umalaya unazidi kuongezeka jamani tuiokoe jamii yetu
 


Hata makelele ya Maimamu misikitini nayo hatuwezi kuendelea kuyavumilia, haiwezekani Ibada ni saa 11 alfajili, Imamu anaanza kutupigia kelele za swaala swaala swaala swaala tangu saa 9 usiku na porojo kibao, eti hiyo shuka ndio sanda yako na hicho kitanda ndio kaburi lako, amkeni amkeni, sasa saa 9 usiku muumini aamke aende kuswali wapi? sina tatizo na adhana zote tano lakini haya makelele nayo ya kuharibiana usingizi sasa hayakubaliki tena. kila anayetaka kuswali alfajili na anunuwe Alarm ya kengele.
 
Yeye analalamikia kelele za huo ukumbi sasa kama gesti za huko kwenu zina kelele toa dukuduku lako na wewe
Gesti zinaweza kuwa na madhara makubwa zaidi ya hizo kelele ndio maana mkuu akamshauri hivyo.
 
Hiyo ni kazi nzuri iliyohaririwa vyema na ERIC SHIGONGO na kudhaminiwa na RIZ-MOKO, kwa pamoja 2nashangweka ndani ya riukumbiiiiiii full kuchangia pato la Taifa .......:israel:...... teh teeh teh teeeeeeehhh
 

Ni kelele ambazo watu wamejitoa fahamu,wanaishi ya enzi ya mawe. Kelele kuanzia saa 9 usiku,na mbaya zaidi sauti ikisambaa kilomita kadhaa kulingana na uwezo wa kipaza sauti. Lazima serikali kwa kushirikiana na viongozi wa dini waweke viwango vya sauti zinazoruhusiwa usiku. Bila hivyo tutaishi kama mahayawani wanavyoishi maporini.
 

Mbona mmehama mada? Mshaingia kwenye azana,ficheni hisia zenu bwana!
 
hahahahahah jf is never boring lol
 
Inaonekana siku hizi hupendi kuingia Dar live kw sababu zako ndo umeanzisha lawama? Ukumbi una muda gani tangu uanzishwe?? kwa hali yoyote wahusika wana leseni na serikali ya mtaa na halmashauri ya manisapaa ikiwemo ofisi ya utamaduni jiji wameruhusu hali halisi inajulikana mona huku lalamika wakati ule unaingia na kujimwaga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…