Kuna kampuni moja ya wahindi kuna bosi mmoja aliwachanganya marafiki pasipo kujijua
Ishu ilikuwa hivi bosi alimwita mmoja wa hao marafiki akamwambia nimesikia rafiki yako ni mwizi akamuomba mchunguze kwa malipo ya 50000,ila asimwambie rafiki yake jamaa kwa tamaa akakubali akasepa,
Kesho yake yule bosi muhindi akamwita yule rafiki mwingine aliyemtuhumu kuwa ni mwizi,kama kawaida muhindi akampanga jamaa akamwambia Ohh nimesikia Rafiki yako kuwa anatabia ya udokozi kama VP naomba umchunguze ila usimwambie, nitakulipa 50000,basi jamaa nae akakubali 😁
Kilichotokea marafiki wawili wanapelelezana pasipo wenyewe kujijua ilikuwa full kupelekeana umbea kwa bosi mwisho wa siku wamekuja kustukia wanachezewa mchezo na kazi wakapigwa chini.