Matatizo yako katika kila sekta na mafanikio pia. Kuna matatizo kwenye kilimo, ufugaji, uvuvi, elimu, maji, ajira, nishati, miundombinu na kadhalika. Kiongozi mzuri ni yule anayetambua mafanikio na kuyatumia kama msingi wa kupambana na matatizo yaliyopo. Wakati wote kutakuwa na matatizo. Maendeleo ni mchakato wa kutatua matatizo na ni mchakato wa kudumu. Hakuna nchi, hata zile ambazo zimeendelea sana, ambazo zimemaliza mchakato wa maendeleo na kumaliza matatizo yote