Mpunilevel
JF-Expert Member
- Sep 14, 2015
- 3,140
- 1,871
Members, Salam!
Naomba tuliweke sawa hili la kauli ya serikali kuhusu upatikanaji wa sukari nchini.
Nakumbuka mheshimiwa Rais Magufuli, kama sinukuu vibaya, alisema, hapo nyuma kwamba sukari imekua ikiagizwa kiholela nchini, hivyo akasema Kunzia siku hiyo vibari vya sukari vitatolewa na watu watatu, akimaanisha Yeye Rais, Makamu wa Rais na waziri mkuu pekee.
Lengo likiwa ni kulinda viwanda vya ndani zidi ya sukari itokayo nje ambayo nyingi iliingia na kuuzwa bei ya chini sana, ikizingatiwa nyingine kuingia bila kulipiwa ushuru, ya magendo. Matokeo yake viwanda vya ndani kushindwa kumudu ushindani wa soko.
Baada ya tamko la waziri mkuu juzi bungeni kutamka kwamba serikali imeagiza sukari, maneno yameanza.
Serikali ilikurupuka kuzuia uagizwaji wa sukari.
Naomba liwekwe wazi na wajuzi wa lugha. Serikali ilizuia jumla uagizwaji wa sukari
au ilizuia uagizwaji wa holela!
Na je? Kweli Kuna upungufu wa sukari nchini? Au Ndio kupima ubavu wa serikali Kuhusu tamko hilo?
Nawasilisha