Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 515
- 2,875
Hujawahi soma chuo nn MKUUUHata hiyo ya wanafunzi kusajiliwa bila kulipa hela yyte bado sijamuelewa naona kama kna ukakasi kidgo hajaweka mkazo.
Bunge limemtaka waziri atoe tamko la serikali kitu ambacho hakiwezi kujadiliwa bungeni. Nilitegemea ile hotuba ingewekwa chini ya darubini lakini ndo imetoka hivyo maisha yanaendelea.mchawi wa mambo yote hayo ni bunge letu kuwa dhaifu. bunge limeiachia serikali ifanye kila kitu itakacho.
Umeweka hii rangi ili usome pekeyako au!!?Nimemsikiliza waziri lakini kuna tatizo la flow ya data zake labda kama bunge wataweka tamko lile kwa maandishi (huenda hakupata muda wa kutosha kupresent alicho andika).
Udahili: Waziri amesema mfumo huu unampatia kila kijana kile anachotaka kwa hiyo wataendelea nao mwakani na kitu watakacho angalia ni jinsi ya kushughulikia multiple selections. Sasa naona waziri amesha amua nini kiendelee kufanyika-nilidhani wana data inayo wawezesha kufanya tathmini kulinganisha mfumo ulio pita na huu wa sasa.
Bado wakiwa na lengo la kumpatia mtu kile apendacho kwani hata mfumo uliopita watu walichagua ingawa inasemekana kuna ambao walipangiwa vyuo/program ambayo hawakutaka. Tujiulize kidogo-ukisha kosa awamu ya kwanza (data za waziri zinaonyesha ni 36 831 walipata round hii, 40 925 walikosa wallichotaka) kwa program na vyuo ulivyo omba bado utasema umepata "ulichotaka" round ya pili au ya tatu? Kwa system ya zamani pia kulikuwa na round ya pili. Je kwa kukubaliana kwamba kila muombaji apewe alicho omba bila kupangiwa kinginecho CAS isingeweza kufanya hivyo na kuhitimisha zoezi kwa muda mfupi zaidi ukizingatia kwamba ingeondoa multiple selections?
Ukimsikiliza waziri hata kama hakutaka kusema sana mfumo wa mwaka huu tatizo kubwa ilikuwa MULTIPLE SELECTIONS bahati mbaya lawama naona katupia vyuo na wanafunzi zaidi. Ingawa data hakutoa lakini ukipiga hesabu (kiujanja ujanja) utaona mwishowe ni zaidi ya wanafunzi 14000 waliokosa vyuo kwa sababu mbali mbali. Sitaki kuamini kuwa hawa wote hawakuwa na sifa. Ukichukua mtizamo wa kitaifa unajiuliza je hili linakubalika. Bahati mbaya waziri hakusema kati ya wale 77 756 walio omba kwanza ni wangapi waliomba bila na kuwa na zile point 4 zinazihitajika.
Wakati wa kuomba round ya pili na ya tatu CAS ilikuwa inaonyesha vyuo vipi na program gani zina nafasi, mfumo wa mwaka huu haukuweza kuonyesha hivyo ikimaanisha watu walichagua wakiwa na upofu katika hili. Na ili mfumo wa mwaka huu uonyeshe hivyo basi mzunguuko wa udahili ungekwenda mpaka December.
Program zenye ushindani ni zipi? Hapa wengi tumetumia hisia zaidi ya ukweli. TCU ingeweza kutoa data inayoashiria program hizo (nafasi zilizopo, kwa wastani huko nyuma wamechukua percentage gani ya waombaji, cutt-off point halisi za mwaka uliopita za hiyo program). Vyuo navyo viweke data hizi kwenye website zao chini ya admission.
Multiple selection: Hili wachangiaji wengi waliliona mara tu baada ya CAS kufutwa. Data ya waziri ilinitatiza aliposema mpaka mwisho walikuwa na 28 466 multiple selections (je hii ni namba ya multiple selections mwisho wa October 2017 au ni jumla ya wote waliopata multiple selections kwenye mchakato mzima?) Kwa vyovyote vile hii namba ni kubwa matokeo yake
(1) kuna walio kosa nafasi kwa sababu ya wenzao walio chaguliwa chuo zaidi ya kimoja (2) Kuchelewa kwa majina kupelekwa HESLB (BODI) na bodi kama hawajui umechaguliwa chuo gani hawakupi mkopo. Ukisikiliza waombaji kuna wanao dai vyuo vimewang'ang'ania wanafunzi, kuna wanafunzi waliconfirm toka round ya kwanza lakini mpaka mwisho wanaambiwa hawaja confirm, kuna wengine tuna ambiwa baada ya kuwa approved na TCU waliendelea kuomba. Je hapa tuna dawa gani, CAS haikuwa na hili. Matokeo yake bodi imetoa maamuzi ya kuwapa wanafunzi 29000+ wakati majina ya wanafunzi wengine wengi (yale yaliyotolewa na TCU mwisho wa October 2017 ) yakiwa hayajafika BODI. Kama serikali iliamua kutoa mikopo kwa 30000 tu hawa wa mwisho wana nafasi gani ya kupata mkopo?
Ni wazi WIZARA, TCU, HESLB, VYUO, TAHLISO na wadau wengine wana kazi kubwa ya kufanya. Ningeshauri tufanye tathmini kwanza ya matokeo ya mwaka huu ndo tuangalie mfumo upi utatufaa. Bahati mbaya waziri inaonekana kesha amua.
Mambo ya jinsi ya kuhandle mikopo vyuoni Abdul Nondo10 (mtoa uzi) ameelezea vizuri. Lakini issue ya kiasi gani kitengwe kwa mikopo bado serikali haijatenga kiasi cha kutosha hasa tunapo ambiwa serikali ni tajiri. Hata kama ni masikini kama hatuwekezi vya kutosha kwenye elimu hatuta toka.
Nimekuwa naitumia kwa zaidi ya miaka 4 sasa. Inakupa shida gani mkuu?Umeweka hii rangi ili usome pekeyako au!!?