Kauli ya Mh.Ndalichako juu ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,873
Majibu ya mikopo kutoka kwa wazir.Mh.Mama Ndalichako.

1.TSNP tulikuwa tunapinga vyuo kudahili baadaye ,kusema Nafasi zimejaa Mfano.chuo cha mwenge university. Ambapo kama mnakumbuka tuliandika barua ya wazi ,kwa naibu wazir na akatatua tatizo hili leo ,tena Mh.wazir amekasirishwa saana na tabia za vyuo hivi.[HASHTAG]#tunakushukuru[/HASHTAG] Mh.wazir.

2.TSNP Tuliwahi kupinga mfumo wa vyuo kuzuia Wanafunzi kusaini fedha zao,za mkopo hadi wamalize usajili,na hili pia tuliwahi mueleza Naibu wazir wa elimu leo pia Mh.wazir ameonesha kukasirika sababu Makubaliano ya mkopo ni wanafunzi na serikali sio chuo,hivyo amekasirishwa na namna vyuo vinavyofanya.hivyo ni kazi ya viongozi wa wanafunzi vyuoni. kusimamia kauli ya Mh.wazir.[HASHTAG]#tunashukuru[/HASHTAG] Mh.wazir.

3.TSNP tulikuwa tunasemea saana na bado tunasemea saana,juu ya idadi ndogo ya wanafunzi mwaka wa kwanza kupewa mkopo wanafunzi elf.30 tuu, Mh.wazir amesema ndio ilikuwa lengo kutoa hao elf 30 hata kabla idadi ya waombaji haijajulikana .,huku mkurugenzi wa bodi Jana akisema hao elf 30 ndio waliochambuliwa na ndio wenye vigezo kati ya elf 61.Wazir anasema lengo ilikuwa wanafunzi elf 30 tuu.[HASHTAG]#hapa[/HASHTAG] sijaelewa [HASHTAG]#tukutane[/HASHTAG] J.mos

Abdul Nondo.
Mkurugenzi idara ya haki
Wajibu wa wanafunzi(TSNP).
0659366125
 
yani wanatoa vipaumbele kwenye vitu vingine wanaacha kuitengea bajeti nzuri elimu
yani nashindwa kuelewa au ni mkakati wa kutengeneza taifa la mambumbu ili waweze kututawala vizuri
maana Tanzania ya viwanda bila wataalam ni bure
 
  • Thanks
Reactions: m2u
Hata hiyo ya wanafunzi kusajiliwa bila kulipa hela yyte bado sijamuelewa naona kama kna ukakasi kidgo hajaweka mkazo.
 
Hujawahi soma chuo nn MKUUU

Kimsingi wazir haez SEMA kila kitu,anaelewa kina hofu nyi kaja.
Wengi wanafinzi huohuo mkopo wakipata hutumia kuongezea ktk ada zao
 
tunashindwaa kufanya usajili ada hatunaaa tunategemea mikopo
 
Nimemsikiliza waziri lakini kuna tatizo la flow ya data zake labda kama bunge wataweka tamko lile kwa maandishi (huenda hakupata muda wa kutosha kupresent alicho andika).

Udahili: Waziri amesema mfumo huu unampatia kila kijana kile anachotaka kwa hiyo wataendelea nao mwakani na kitu watakacho angalia ni jinsi ya kushughulikia multiple selections. Sasa naona waziri amesha amua nini kiendelee kufanyika-nilidhani wana data inayo wawezesha kufanya tathmini kulinganisha mfumo ulio pita na huu wa sasa.

Bado wakiwa na lengo la kumpatia mtu kile apendacho kwani hata mfumo uliopita watu walichagua ingawa inasemekana kuna ambao walipangiwa vyuo/program ambayo hawakutaka. Tujiulize kidogo-ukisha kosa awamu ya kwanza (data za waziri zinaonyesha ni 36 831 walipata round hii, 40 925 walikosa wallichotaka) kwa program na vyuo ulivyo omba bado utasema umepata "ulichotaka" round ya pili au ya tatu? Kwa system ya zamani pia kulikuwa na round ya pili. Je kwa kukubaliana kwamba kila muombaji apewe alicho omba bila kupangiwa kinginecho CAS isingeweza kufanya hivyo na kuhitimisha zoezi kwa muda mfupi zaidi ukizingatia kwamba ingeondoa multiple selections?

Ukimsikiliza waziri hata kama hakutaka kusema sana mfumo wa mwaka huu tatizo kubwa ilikuwa MULTIPLE SELECTIONS bahati mbaya lawama naona katupia vyuo na wanafunzi zaidi. Ingawa data hakutoa lakini ukipiga hesabu (kiujanja ujanja) utaona mwishowe ni zaidi ya wanafunzi 14000 waliokosa vyuo kwa sababu mbali mbali. Sitaki kuamini kuwa hawa wote hawakuwa na sifa. Ukichukua mtizamo wa kitaifa unajiuliza je hili linakubalika. Bahati mbaya waziri hakusema kati ya wale 77 756 walio omba kwanza ni wangapi waliomba bila na kuwa na zile point 4 zinazihitajika.

Wakati wa kuomba round ya pili na ya tatu CAS ilikuwa inaonyesha vyuo vipi na program gani zina nafasi, mfumo wa mwaka huu haukuweza kuonyesha hivyo ikimaanisha watu walichagua wakiwa na upofu katika hili. Na ili mfumo wa mwaka huu uonyeshe hivyo basi mzunguuko wa udahili ungekwenda mpaka December.

Program zenye ushindani ni zipi? Hapa wengi tumetumia hisia zaidi ya ukweli. TCU ingeweza kutoa data inayoashiria program hizo (nafasi zilizopo, kwa wastani huko nyuma wamechukua percentage gani ya waombaji, cutt-off point halisi za mwaka uliopita za hiyo program). Vyuo navyo viweke data hizi kwenye website zao chini ya admission.

Multiple selection: Hili wachangiaji wengi waliliona mara tu baada ya CAS kufutwa. Data ya waziri ilinitatiza aliposema mpaka mwisho walikuwa na 28 466 multiple selections (je hii ni namba ya multiple selections mwisho wa October 2017 au ni jumla ya wote waliopata multiple selections kwenye mchakato mzima?) Kwa vyovyote vile hii namba ni kubwa matokeo yake

(1) kuna walio kosa nafasi kwa sababu ya wenzao walio chaguliwa chuo zaidi ya kimoja (2) Kuchelewa kwa majina kupelekwa HESLB (BODI) na bodi kama hawajui umechaguliwa chuo gani hawakupi mkopo. Ukisikiliza waombaji kuna wanao dai vyuo vimewang'ang'ania wanafunzi, kuna wanafunzi waliconfirm toka round ya kwanza lakini mpaka mwisho wanaambiwa hawaja confirm, kuna wengine tuna ambiwa baada ya kuwa approved na TCU waliendelea kuomba. Je hapa tuna dawa gani, CAS haikuwa na hili. Matokeo yake bodi imetoa maamuzi ya kuwapa wanafunzi 29000+ wakati majina ya wanafunzi wengine wengi (yale yaliyotolewa na TCU mwisho wa October 2017 ) yakiwa hayajafika BODI. Kama serikali iliamua kutoa mikopo kwa 30000 tu hawa wa mwisho wana nafasi gani ya kupata mkopo?

Ni wazi WIZARA, TCU, HESLB, VYUO, TAHLISO na wadau wengine wana kazi kubwa ya kufanya. Ningeshauri tufanye tathmini kwanza ya matokeo ya mwaka huu ndo tuangalie mfumo upi utatufaa. Bahati mbaya waziri inaonekana kesha amua.

Mambo ya jinsi ya kuhandle mikopo vyuoni Abdul Nondo10 (mtoa uzi) ameelezea vizuri. Lakini issue ya kiasi gani kitengwe kwa mikopo bado serikali haijatenga kiasi cha kutosha hasa tunapo ambiwa serikali ni tajiri. Hata kama ni masikini kama hatuwekezi vya kutosha kwenye elimu hatuta toka.
 
Vyuo vingine viliwachagua tena awamu ya pili wale ambao ziliwaacha awamu ya kwanza kwa kuwasingizia eti wameomba tena, lakini wakiwa wamechaguliwa na vyuo vingine awamu ya kwanza na wameconfirm vyuo hivyo! Mzumbe, University of Iringa etc walifanya hivyo!
 
mchawi wa mambo yote hayo ni bunge letu kuwa dhaifu. bunge limeiachia serikali ifanye kila kitu itakacho.
 
Bunge limemtaka waziri atoe tamko la serikali kitu ambacho hakiwezi kujadiliwa bungeni. Nilitegemea ile hotuba ingewekwa chini ya darubini lakini ndo imetoka hivyo maisha yanaendelea.
 
Nimemsikiliza waziri lakini kuna tatizo la flow ya data zake labda kama bunge wataweka tamko lile kwa maandishi (huenda hakupata muda wa kutosha kupresent alicho andika).

Udahili: Waziri amesema mfumo huu unampatia kila kijana kile anachotaka kwa hiyo wataendelea nao mwakani na kitu watakacho angalia ni jinsi ya kushughulikia multiple selections. Sasa naona waziri amesha amua nini kiendelee kufanyika-nilidhani wana data inayo wawezesha kufanya tathmini kulinganisha mfumo ulio pita na huu wa sasa.

Bado wakiwa na lengo la kumpatia mtu kile apendacho kwani hata mfumo uliopita watu walichagua ingawa inasemekana kuna ambao walipangiwa vyuo/program ambayo hawakutaka. Tujiulize kidogo-ukisha kosa awamu ya kwanza (data za waziri zinaonyesha ni 36 831 walipata round hii, 40 925 walikosa wallichotaka) kwa program na vyuo ulivyo omba bado utasema umepata "ulichotaka" round ya pili au ya tatu? Kwa system ya zamani pia kulikuwa na round ya pili. Je kwa kukubaliana kwamba kila muombaji apewe alicho omba bila kupangiwa kinginecho CAS isingeweza kufanya hivyo na kuhitimisha zoezi kwa muda mfupi zaidi ukizingatia kwamba ingeondoa multiple selections?

Ukimsikiliza waziri hata kama hakutaka kusema sana mfumo wa mwaka huu tatizo kubwa ilikuwa MULTIPLE SELECTIONS bahati mbaya lawama naona katupia vyuo na wanafunzi zaidi. Ingawa data hakutoa lakini ukipiga hesabu (kiujanja ujanja) utaona mwishowe ni zaidi ya wanafunzi 14000 waliokosa vyuo kwa sababu mbali mbali. Sitaki kuamini kuwa hawa wote hawakuwa na sifa. Ukichukua mtizamo wa kitaifa unajiuliza je hili linakubalika. Bahati mbaya waziri hakusema kati ya wale 77 756 walio omba kwanza ni wangapi waliomba bila na kuwa na zile point 4 zinazihitajika.

Wakati wa kuomba round ya pili na ya tatu CAS ilikuwa inaonyesha vyuo vipi na program gani zina nafasi, mfumo wa mwaka huu haukuweza kuonyesha hivyo ikimaanisha watu walichagua wakiwa na upofu katika hili. Na ili mfumo wa mwaka huu uonyeshe hivyo basi mzunguuko wa udahili ungekwenda mpaka December.

Program zenye ushindani ni zipi? Hapa wengi tumetumia hisia zaidi ya ukweli. TCU ingeweza kutoa data inayoashiria program hizo (nafasi zilizopo, kwa wastani huko nyuma wamechukua percentage gani ya waombaji, cutt-off point halisi za mwaka uliopita za hiyo program). Vyuo navyo viweke data hizi kwenye website zao chini ya admission.

Multiple selection: Hili wachangiaji wengi waliliona mara tu baada ya CAS kufutwa. Data ya waziri ilinitatiza aliposema mpaka mwisho walikuwa na 28 466 multiple selections (je hii ni namba ya multiple selections mwisho wa October 2017 au ni jumla ya wote waliopata multiple selections kwenye mchakato mzima?) Kwa vyovyote vile hii namba ni kubwa matokeo yake

(1) kuna walio kosa nafasi kwa sababu ya wenzao walio chaguliwa chuo zaidi ya kimoja (2) Kuchelewa kwa majina kupelekwa HESLB (BODI) na bodi kama hawajui umechaguliwa chuo gani hawakupi mkopo. Ukisikiliza waombaji kuna wanao dai vyuo vimewang'ang'ania wanafunzi, kuna wanafunzi waliconfirm toka round ya kwanza lakini mpaka mwisho wanaambiwa hawaja confirm, kuna wengine tuna ambiwa baada ya kuwa approved na TCU waliendelea kuomba. Je hapa tuna dawa gani, CAS haikuwa na hili. Matokeo yake bodi imetoa maamuzi ya kuwapa wanafunzi 29000+ wakati majina ya wanafunzi wengine wengi (yale yaliyotolewa na TCU mwisho wa October 2017 ) yakiwa hayajafika BODI. Kama serikali iliamua kutoa mikopo kwa 30000 tu hawa wa mwisho wana nafasi gani ya kupata mkopo?

Ni wazi WIZARA, TCU, HESLB, VYUO, TAHLISO na wadau wengine wana kazi kubwa ya kufanya. Ningeshauri tufanye tathmini kwanza ya matokeo ya mwaka huu ndo tuangalie mfumo upi utatufaa. Bahati mbaya waziri inaonekana kesha amua.

Mambo ya jinsi ya kuhandle mikopo vyuoni Abdul Nondo10 (mtoa uzi) ameelezea vizuri. Lakini issue ya kiasi gani kitengwe kwa mikopo bado serikali haijatenga kiasi cha kutosha hasa tunapo ambiwa serikali ni tajiri. Hata kama ni masikini kama hatuwekezi vya kutosha kwenye elimu hatuta toka.
Umeweka hii rangi ili usome pekeyako au!!?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom