tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla ameomba ushirikiano kutoka kwa viongozi na wananchi ili kuendeleza shughuli za kiuchumi zikiwemo sekta ya utalii na kilimo cha maua na mbogamboga.
Akizungumza leo Ijumaa, Agosti 29, 2025 baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwaajili ya kuanza majukumu yake baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan amesema anao uzoefu wa kutosha kutekeleza kazi aliyopewa aifanye.
Soma pia: Kenani Kihongosi ateuliwa kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi, na Mafunzo akichukua nafasi ya Amos Makalla
Makalla amechukua nafasi hiyo akipokea kijiti kutoka kwa mtangulizi wake Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi.
Amesema amekwenda Arusha kuitimiza mazuri yote yaliyofanywa na viongozi waliomtangulia na hivyo atayaendeleza kwa masilahi mapana ya wananchi.
Makalla amesema atatumia uzoefu alioupata akiwa mkuu wa mikoa mitano ya Kilimanjaro, Mbeya, Katavi, Dar es Salaam na Mwanza kuhimiza shughuli za kiuchumi kwa wananchi na kuhimiza viongozi kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi huko walipo.