Katika filamu ya Sarafina, nimeukumbuka ule wimbo wa SABELA

Chawa wa lumumbashi

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
793
1,749
SABELA

Katika filamu ya Sarafina, nimeukumbuka ule wimbo wa SABELA. Huwa naupenda sana. Napenda sauti zao na beats zake.

Kuna wakati unajikuta unaupenda wimbo hata pasipo kujua maana yake. Tena unaweza ukausikiliza ukakugusa hadi kwenye kongosho. 😛

Leo nawaimbisha kizulu wallah! 😁😁
Nimejaribu kukuwekea tafsiri isiyo rasmi ili uburudike zaidi.

🎤🎤🎤🎤🎤🎵🎵🎶🎶
Uhlala ngabantw' emabhunwini babo! Uyaziqeketh' izindaba ngabantu x2
Uhola ngegazi labantu U-R100 igazi lendoda
Ubaqedile bo! Baphelile Laf' elikamjokwane kandaba x2

☀Unapeleka habari za watu kwa makaburu, unaongelea mambo ya watu
Unafaidika damu ya mtu inapomwagika, randi 100 kwa damu ya binadamu mwenzio
Umewamaliza, ubinadamu unaharibiwa

Izimpimmpi zonke zigcwel' umhlaba zisidiqedile. Helele!
Weh may babo! Oh laf' elikamjokwane kandaba x2
ESiya stradi hoo bakhuluma ngawe
Kanti nase Pitoli bayakukhokhela
Ukhonjwa ngegama ngapha nangapha izwelonkebo
ESoweto, kwaMhash' eMlazi ubaqedile
Wo bamb' uqede bo!

☀Wapeleka habari/ wapelelezi duniani kote wametumaliza.
Ooh Jamani! Ubinadamu unaharibiwa.
Kila mtu anakuongelea wewe mtaa wa Siya
Hata huko Pretoria, wanakulipa wewe
Wanakunyooshea vidole na kulitaja jina lako, kote huko
pale Soweto, Mhashu na Mlazi, umewamaliza wewe.
Tafadhali acha sasa!

Hiki kipande huwa kipo zaidi kwenye Audio yake.
Mbambeeeen' uSabela, Ubaqedile
Oh laf' elikamjokwane kandaba

☀Mkamateni Sabela, amewamaliza wenzake
ubinadamu unaharibiwaaa

Nite nite friends...
Ni wimbo gani unaupenda zaidi kwenye filamu ya Sarafina?

Lyrics: kwa msaada wa mitandao.
 
Back
Top Bottom