Katika ajira za Walimu 6000 Ile orodha walioichukua mwaka jana waliifanyia kazi? Mrejesho wake ukoje?

Mathias_95

Member
Apr 17, 2021
26
80
Ndugu wanajamvi nasikitika kusema kwamba lile zoezi la kuandika majina ya waalimu wanaojitolea limeanza kujirudia tena kama ilivyokuwa mwaka jana.

Binafsi sipingani na hoja ya kuwapa kipaumbele vijana wanaojitolea, lakini ninamaswali machache tu;

1. Ile list walioichukua mwaka jana waliifanyia kazi? Mrejesho wake ukoje?

2. Kama wameamua kuchukua list nyingine ilihali hiyo ya mwaka jana hawajaifanyia kazi hawaoni watakuwa hawajafanya fair kwa vijana waliojitolea kwa muda mrefu wakavunjika moyo baada ya kutojumuishwa kwenye ajira 8,000 wakaamua kutafuta angalau vibarua vya kufanya?

ALL IN ALL, URASIMU, CONNECTION NA MATUMIZI YA FEDHA KUPATA AJIRA HUANZIA HAPA.

Sisi wengine tusio na connection tuendelee kutulia
View attachment 1762219
 
Back
Top Bottom