Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, azuia barua za Uteuzi wa Wagombea wa CCM , Udiwani Kata na Viti Maalum kwa Majimbo 8,isipokuwa Moshi Mjini

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
16,029
Reaction score
26,231
Katika kikao cha hivi karibuni cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kilimanjaro, katibu wa mkoa, Mercy, alikabiliwa na hali ya kushangaza na kusikitisha.

Kikao hicho kilikuwa na jukumu la kukutana na kupitisha majina ya wagombea wa udiwani wa kata na viti maalum kwa kata mbalimbali za mkoa huo.

Hata hivyo, uamuzi wa kuzuia kutangazwa kwa majina ya wagombea hao umesababisha sintofahamu miongoni mwa wanachama na viongozi wa CCM.

Mercy , ambaye ni katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, alikataa kutangaza majina ya walioteuliwa na pia kuzuia kuwapatia barua za uteuzi wagombea kutoka majimbo ya Same Mashariki, Same Magharibi,Mwanga, Rombo, Hai, Siha, Vunjo, na Moshi Vijijini.

Katika hali isiyo ya kawaida, aliruhusu tu majina ya wagombea kutoka Jimbo la Moshi Mjini kutangazwa na kuwapatia barua zao za uteuzi.

Hali hii imeibua maswali mengi kuhusu uwazi na haki katika mchakato wa uteuzi wa wagombea.

Tukio hili linatia wasiwasi mkubwa na linaweza kuathiri mchakato mzima wa uchaguzi.

Wanachama wa CCM wanajiuliza ni kwa nini majimbo mengine hayakupata nafasi sawa katika kutangazwa kwa wagombea wao, wakati kikao cha Halmashauri Kuu kilikamilika na kupitisha majina hayo.

Hali hii ya ukimya inazua maswali zaidi kuliko majibu, na wengi wanashindwa kuelewa ni nini hasa kinachosababisha tofauti hii katika uteuzi.

Tunamwomba Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Balozi Nchimbi, kufuatilia hali hii kwa karibu.

Ni muhimu kujua sababu zilizofanya majimbo mengine ya Mkoa wa Kilimanjaro kuzuia wagombea wao kupata barua za uteuzi, wakati kikao halali cha Halmashauri Kuu kilishaidhinisha majina hayo.

Je, kuna sababu maalum zinazofanya hawa wagombea wawe na kibali tofauti?

Wakati tulipompigia simu Mecry ,ili kupata ufafanuzi, alikataa kujibu maswali yetu na kuelekeza suala hilo kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa, akizima simu yake ya mkononi.


Hali hii ya kutokuwa na uwazi inatia shaka kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi na jinsi ambavyo viongozi wanavyoshughulikia masuala haya nyeti.

Kila mwanachama wa CCM anatarajia mchakato wa uchaguzi uwe wa haki na uwazi, ambapo kila mgombea anapata fursa sawa.

Kuzuia kutangazwa kwa majina ya wagombea ni hatua inayoweza kuharibu imani ya wanachama katika chama. Ni muhimu kwa viongozi wa CCM kuhakikisha kuwa kila hatua inachukuliwa kwa uwazi na haki ili kuimarisha chama na kujiandaa vizuri kwa uchaguzi ujao.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…