Akiongea na waandishi wa habari, wakati akijibu swali kutoka kwa waandihshi juu ya maoni yake kuhusu CCM kutufikisha katika hali hii ya kuibiwa, katibu mwenezi wa ccm amesema kuulizana hivyo i sawa na kuulizana kwamba mwaka 1978 nduli alikuwa sahihi ama la!. Hii ni kukiri kwamba CCM ni nduli kwa Watanzania na hakuna sababu yakujadili hoja hiyo ya kwamba ccm imeliangusha taifa, badala yake tuungane tupigane vita dhidi ya nduli!.
Hata hivyo, ameonyesha hofu ya kuinyoshea vidole serikali kwa kushindwa kwake mojakwa moja na badala yake ametupia mpira wawekezaji kwa ku understate thamani za madnii kwenye mchanga. Hii inaonyesha moja kwa moja kwamba serikali haina control measures zaidi ya ku rely totally kwenye taarifa za mfanya biashara. Kwa hiyo hakuna supervisory services kutoka serikali na hiyov kuzidi kuifanya TZ shamba la bibi.
Kuhusiana na mauaji yanayoendelea kibiti, amelaumu vyama vya upinzani kwamba vinafanya siasa ya madaraka badala ya siasa za maendeleo, kiasi cha kukaa kimya badala ya kuonyesha ushirikiano katika kulinda maslahi ya taifa. Mheshimiwa Polepole inaonekana anasahau kwamba:-
1 Chama chake ndicho kilichopiga marufuku vyama vingine kufanya siasa na hakuna chama kinafanya siasa zaidi ya ccm. Sasa labda ccm iruhusu vyama vingine pia vifanye siasa ili viisaidie ccm katika control kwa kuwa sasa ni dhahiri Ccm imeshindwa.
2. Mheshimiwa amesahau kwamba mambo ya kupotea uhai wa binadamu vimekuwa vikitokea mfn, Mauaji ya Kamanda Mawazo, upotevu wa Ben Saanane, ikiwa ni pamoja na matukio mbalimbaliambayo yanaashiria ukiukiwaji mkubwa wa haki za binadamu. Lakini hatujaona juhudi za pamoja za vyama vya siasa vikishikamana katiak kukomesha uharifu huo. Ninachokiona kinachoweza kutusaidia, ni kuimarisha mshikamano katika mambo yote. Hii ni dalili mbaya sana ya mgawanyiko na matabaka katika nchi, ambayo imeasisiwa lakini inaweza kabisa kurekebishwa na Ccm na wengine wakafuata.
SASA KWA MANTIKI HII KWAMBA CCM NI NDULI NA NDIYE KATUFIKISHA HAPA, CCM INAJITAMBUA KI HIVYO?
VITA VYA KUPAMBANA NA NDULI HUYU, VINAWEZA KUWA NA CHANGAMOTO KWA KUWA NDULI YUKO KATIKATI YETU. ANAPASHWA KUJITAMBUA NA MARA MOJA KUDHAMIRIA KUBADILIKA, KAMA AMEONA UNDULI WAKE NDIYO UNAOLETA MAUMIVU KWA TAIFA.
BILA CCM KUJITMBUA NA KUBADILIKA, VITA HIVI NI VIGUMU NA VINAGHARAMA KUBWA.
Sijui wenzangu mnaonaje